.

.

.

.

Wednesday

Mwanamke aliyeasi Dini akamatwa tena

Taarifa kutoka nchini Sudan zinasema kuwa mwanamke aliyeachiliwa hapo juzi kwa kosa la kuasi dini amekamatwa tena.

Mwanamke huyo Meriam Ibrahim, alikuwa amehukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mwanamume mkristo na kukana dini ya kiisilamu alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja wa ndege mjini Khartoum.
Merian na familia yake Sudan

Watu waliomkata walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia ingawa wanaaminika kuwa wanajeshi wa serikali.

Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake.

Haijulikani kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.Meriam alikamatwa kwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela baada ya kuhukumiwa.

Alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake msichana jela punde baada ya kuhukumiwa.

Familia yake imepelekwa katika makao makuu ya idara ya ujasusi.Kabla ya kuzuiliwa kwaketena, jamii ya kimataifa yalipongeza uamuzi wa kuachiliwa kwake na kumuondolea hukumu ya kifo chake.

No comments:

Post a Comment