.

.

.

.

Tuesday

TCRA YASISITIZA MATUMIZI SAHIHI NA SALAMA YA MITANDAO NCHINI

Katika kupambana na makosa ya uhalifu wa kimtandao nchini TCRA kwa kushirikiana na kampuni ya Kingdom Heritage ilifanya semina kwa vijana yenye lengo la kuwajengea uelewa wa namna nzuri ya matumizi na usalama Mtandao.

Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwaka wiki iliyopita katika ukumbi wa Buni Hub tume ya Sayansi Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vijana kutoka vyuo na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.

Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe alipokuwa akizungumza katika warsha hiyo alisema  kulingana na ukuaji wa miundombinu ya TEHAMA inakuwa kwa kasi na kusababisha matokeo chanya na hasi katika jamii zetu
“Katika majira haya ya maendeleo ya TEHAMA waharifu wanatumia mwanya huo kufanya uharifu katika mifumo mbali mbalimbali ya Kompyuta hivyo tunatakakiwa kuwa makini kwa watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA nchini,” alisema Dk Filikunjombe.

Alisema kama TCRA wanazidi kusisitiza kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao tena yenye maadili ili kupunguza uhalifu huo, Kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao.

Mwanzilishi wa Jamii Forums na muwasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo alizungumzia fursa mbalimbali zinazopatikana katika mitandao na miundombinu ya TEHAMA kwa kuwasihi vijana waliokuwa hapo kuwa wabunifu katika majira haya na kuja na mifumo suluhisho itakayoweza kutumika katika jamii zetu.

“Serikali pia kupitia wizara au mamlaka zinazohusika kusapoti juhudi za vijana wabunifu katika TEHAMA  kwa miundombinu na kanuni na taratibu rafiki ili waweze kujifanikisha katika ubunifu wao mpaka kijipatia kipato binafsi na taifa zima kwa ujumla.” Alisema Melo.

Mtaalamu wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya Kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu alizungumzia  namna ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kimtandao na kuwa salama mtandaoni.

“Nchi nyingi za Afrika tunakosa uelewa wa maarifa ya kujilinda na mashambulizi ya kimtandao na kupelekea kupata hasara sana katika taasisi au watu binafsi kutokana na mashambulizi hayo,” alisema Matafu.

Aliongeza “Takwimu zinaonyesha taasisi nyingi afrika na Tanzania tukiwepo hatuwekezi vya kutosha katika mifumo ya kiulinzi na usalama mtandao,kwa kufanya hivyo tunaongeza asilimia kubwa za kupata mashambulizi ya kimtandao katika tasisi zetu,” alisema.

Awali, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela alisema wao kwa sehemu yao wanaunga mkono juhudi za serikali kupitia TCRA katika kupambana na makosa ya uharifu wa kimtandao kwa kutoa elimu kwa umma hasa vijana ambao ndio rika linalotumia sana mitandao.

“Ili kujua matumizi sahihi na salama vijana mliopo hapa lazima mtambue kuwa sheria ya makosa ya uhalifu wa kimtandao ipo na inafanya kazi lazima tuheshimu na kutii vitu inavyotuzuia kufanya bali tutumie mitandao kwa namna za ubunifu zenye kutuletea fedha na kujiingizia kipato,” alisema Bashemela.Mwanansheria mwandamizi kutoka TCRA, Dk Philip Filikunjombe

Mwanzilishi wa Jamii Forums mmoja kati ya wawasilishaji mada katika warsha hiyo, Maxence Melo
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kingdom Heritage ambao ndio waandaaji wa semina hiyo Tunu  Bashemela
Vijana mbalimbali watumiaji wa mitandao na wadau wa TEHAMA waliohudhulia semina hiyo wakifuatilia kwa makiniMtaalamu na Mshauri wa masuala ya ulinzi katika mfumo ya kompyuta na TEHAMA nchini kutoka Kampuni ya Kabolik, Robert Matafu katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
  Mtendaji Mkuu wa tzNIC  Abibu Ntahigiye katika mjadala wa katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.
Mwanzilishi wa Jamii Forums katika mjadala na nini kifanyike ili kupunguza na kukomesha matukio ya uhalifu wa mtandao nchini.

Friday

Kingdom Heritage Presents Discover Your Potential
Kampuni ya KINGDOM HERITAGE imeandaa event inaitwa "Discover Your Potential" ni event yenyewe wazungumzaji wahamasishaji katika mambo ya mipango,maendeleo,ndoto na maono na ujasiliamali.

Watakuwa wakizungumza mambo kadhaa yatakayotukumbusha kutambua uwezo wetu tulio nao kila mmoja wetu kwa ulivyo na mahala ulipo na namna ya kuutumia uwezo huo ili kufikia Malengo,Mipango,Ndoto na Maono kila mmoja.

Ni Jumapili wiki hii ya 30 April 2017 katika Kanisa la Living Water Centre Kawe Kuanzia saa 9:00 mchana.Usipange kukosa! ni Bureee!

Thursday

TAMASHA LA SIFA ZA YERIKO ARUSHA
Miaka 25 ijayo, Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii inamaanisha nguvu kazi kubwa itakuwa mikononi mwao, Lakini kama watasalia kuwa idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa kwa ukuaji wa nchi.

Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye makusanyiko ya kijamii mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa nguvu. Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.

Uwepo wa Tamasha la Sifa za Yeriko ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Maono Foundation Limited na washirika wake kuwa sehemu ya kutatua matatizo haya kwa kuanzisha kituo cha ukuzaji wa vipaji kwa vijana, kusudi waweze kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto kwenye jamii.Mkakati wa muda mfupi, ni kuhudumia moja ya kituo cha watoto yatima cha Guardian Angels House of Hope chenye uhitaji wa taaluma za watoto kukuzwa,lakini changamoto ikawa kukosekana kwa ada na mahitaji mengine ya shuleni.Kwa kujumuika kwenye tamasha hili, si tu kwamba watakuwa wanamuaibisha mwovu shetani kwa kuangusha ngome zinazowasumbua kwenye Nyanja mbalimbali maishani, bali pia watakuwa wamechangia katika kutimia kwa malengo ya Maono Foundation.

Tamasha la Sifa za Yeriko msimu wa kwanza inatarajiwa kufanyika tarehe 9 Disemba 2016 Jijini Arusha kwenye Kanisa la New Life City Church (Kwa Egon) lililoko Kwa Iddi, na kisha kufuatiwa na Tamasha la pili litakalofanyika tarehe 11 Disemba Kanisa la Tanzania Assemblies of God CCC Upanga Jijini Dar es Salaam ikiwa ni weekend hii. Tamasha hili litahusishwa waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania, ambapo ugeni kutoka Afrika Kusini utakuwepo. Wageni hawa ni Mercy Manqele, KgotsoMakgalema na Sipokazi Nxumalo.Baadhi ya waimbaji wa ndani ni kama vile, Abednego na The Worshippers, Toddlers International, Yusuphu Nahashon, Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama,Wengine ni Machalii wa Yesu, The Cahogoz, Voice of Joy, Lilian Kimola, na Bomby Johnson.

LENGO
Lengo la awali nikukusanya kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo zitatumika
kutafuta eneo la kituo kwa jijini Dar es Salaam na Arusha, pamoja na matengenezo iwapo itanunuliwa nyumba na kuibadilisha kuendana na maono ya jinsi kituo tunavyotaka kiwe kukidhi mambo mbalimbali yatakayokuwa yakipatikana kituoni, kama kujifunza muziki, uimbaji, ushauri nasaha, na utafutaji wa shule za kukuza vipaji ndani na nje ya nchi.ambayo tunatarajia yatawezesha kupatikana kwa kiasi hiki ni kupitia barua za mwaliko kwa watumishi mbalimbali wa dini na taasisi, pamoja na kiingilio kitakachopatikana kupitia matamasha yote mawili.

GHARAMA
Ili lengo la kukusanya milioni 200 kutimia, gharama mbalimbali kutoka kwa waanzilishi na marafiki zimefanikisha katika kuwakaribisha waimbaji hawa kutoka Afrika Kusini, kulipia mahala watakapofikia, matangazo, usafiri wa ndani, chakula, vyombo, muziki na gharama nyinginezo. Hili litasaidia katika ukusanyaji wa kiasi kilichosalia kwa awamu tofauti tofauti. Tunaamini katika ushirikiano katika kutatua matatizo yaliyomo kwenye jamii yetu

Katika Kufanikisha na maono ya kupata fedha katika Tamasha hilo kwa Dar es salaam na Arusha kutakuwa na Kiingilio katika Matamsha hayo,Arusha ni Ijumaa hii Dec 9 pale kwa Egon Wakubwa 5000 VIP 20000 Dar es salaam ni Jumapili hii Dec 11 pale CCC Upanga Opp Chuo cha Mzumbe Watoto 5000 Wakubwa 10000 VIP 30000


Tunategemea support yenu wadau wa vyombo vya habari Bloggers kwa kwa ajili ya kusaidia kutangaza Tamasha hili linalofanyika lengo na maono tuliyo nayo mbele yetu Arusha na Dar es salam kwa wikendi hii.