.

.

.

.

Monday

Kanisa lawabana wajumbe Bunge la Katiba

Jaji Joseph Warioba
Kanisa la Pentecostal Holiness Association Mission Tanzania (PHAM) limelitaka Bunge Maalumu la Katiba kuhakikisha wanajadili rasimu ya katiba yenye maoni ya wananchi na siyo vinginevyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Askofu wa Kanisa hilo, Julius Bundala, jana wakati wa ibada ya Jumapili, iliyofanyika kwenye kanisa hilo lililopo Makole mjini hapa.

Bundala alisema licha ya kanisa kuliombea taifa na Bunge Maalumu la Katiba, ni vyema Bunge hilo likajadili rasimu ya katiba, ambayo iliwasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.

Alisema ili kuondokana na migogoro isiyokuwa na tija katika nchini ni vyema makundi yote, ambayo yanabishania kuhusu katiba mpya wakakaa mezani na kuondoa tofauti zao.

“Pia ikumbukwe kuwa kinachotakiwa kujadiliwa katika Bunge Maalum la Katiba ni Rasim ambayo inabeba maoni ya wananchi na wala siyo matakwa ya vyama vya siasa.

“Ikumbukwe kuwa Bunge Maalum limetumia muda mwingi kuadaa kanuni kwa ajili ya kuwaongoza sasa inakuwaje watu hao ambao walitunga kanuni wenyewe wanadiliki kuzivunja” alihoji Askofu.

Alisema iwapo kila upande wa wajumbe wa katiba ikiwa wataendelea na misimamo yao bila kupata mwafaka ni wazi kuwa watakuwa wanaendeleza mpasuko kwa kuwagawa Watanzania.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment