.

.

.

.

Friday

PENUEL CONFERENCE 2016



PENUEL Maana yake ni mahala pa Kukutana na Mungu uso kwa uso na nafsi yako ikabaki salama, hii ni kulingana na Mwanzo 32:30 kwa kile kilicho mtokea Yakobo,Kongamano la Penuel linamahanisha mahala pa kukutana na Mungu kupitia Neno lake linalo hubiriwa na watumishi wake mbalimbali kulingana na maelekezo juu ya watu wa Mungu!

Katika Kongamano hili la PENUEL 2016 litajumuisha wanenaji kutoka nje ya Tanzania na ndani ikiwemo Arusha,Afrika Kusini,Mbeya, DRC, Kenya, Cameroon n.k

Mwenyeji wa PENUEL 2016 Apostle Onesmo Ndegi na Lilian Ndegi. Pia wanenaji wengine kutoka Tanzania ni Askofu Emmanuel Tumwidike kutoka Mbeya na Bishop Olam Mustapha kutoka Arusha. Kutoka Kenya ni Bishop Tengu Yoka na kutoka Africa Kusini ni Dr.Apostle Peter Muteba pia kutoka Cameroon tunaye Bishop Angela Acha-Morfaw na Apostle Israel Abam kutoka Nigeria.

Mahali ni Living Water Centre Kawe, Dar es salaam, Tanzania Uzinduzi wa Kongamano ilikuwa ni leo siku ya Jumanne kuanzia saa 8:00 mchana,siku zinazofuata ni kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 12 Jioni.Karibu Ukutane na Mungu kupitia Neno kupitia watumishi wake! Barikiwa!

Theme: Transformation Romans 12:2


 Source:gospelhabari.blogspot.com

No comments:

Post a Comment