.

.

.

.

Tuesday

KUKUA/ KUONGEZEKA KATIKA UFAHAMU WA KIMUNGU kutoka Facebook Church Of All Nations (FBAON)

Neno UFAHAMU ni msamiati wa lugha ya Kiswahili wenye maana ya ujuzi/maarifa. Kwa context ya Biblia hapa tunamaanisha ufahamu wa KIMUNGU AMBAO UNATOKANA NA KULISOMA NA KULIELEWA VEMA NENO LA MUNGU.

Mtu anapomwamini Yesu Kristo moja kati ya mabadiliko yanayotarajiwa ni kufunguliwa kwa ufahamu wake ambao ndio chanzo cha badiliko la kweli ndani yake.


Hosea 4:6a " Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;"
Ufahamu wa mwanadamu ndio pekee unaofunguliwa na MUNGU na mengine yote ni matokeo ya kufunguliwa ufahamu.


Ni lazima tutambue kwamba Ukristo ni suala la mapinduzi ya ufahamu. Tunapompata Yesu tunahitaji ufahamu ndani yetu ambao ni lazima uendelee kukua siku hadi siku.Cha msingi ni lazima pia tutambue kwamba suala la kukua kwa ufahamu wetu ni suala la JUHUDI/JITIHADA BINAFSI.


TUNAPATAJE MAARIFA YA MUNGU?
Warumi 10:17 " Basiimani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa Neno la Kristo"
Wokovu wetu unaambatana na imani ambayo inajengwa kwa kusikia Neno SAHIHI la MUNGU.Kusikia Neno la Mungu ni chanzo cha kujengwa kwa imani yetu. IMANI ni hali ya kuwa na uhakika kwa 100%/ kukubaliana na Neno la Mungu. Kwa ujumla ufahamu wetu unajengwa pia na kiwango cha imani iliyo ndani yetu. 


Ufahamu wa Kimungu ni muhimu sana kwa sababu pasipo ufahamu wa Mungu haiwezekani kufanya mapenzi ya Mungu.Na kukataa maarifa ya Mungu ni kukataa USHIRIKA NA MUNGU.
Kukosa maarifa ya Mungu ni UTUMWA

Isaya 5:13 " Kwa sababu hiyo watu wangu amechukuliwa mateka , kwa kukosa kuwa na maarifa ;".
Tutambue kwamba kweli ya Mungu ndiyo inayotuweka huru.
Hekima ya Mungu (maarifa/ ufahamu) inazaliwa kwa uweza wa ROHO MTAKATIFU akaaye ndani.
Kwa njia ya Neno la MUNGU nia zetu zinaweza kugeuzwa upya/ kufanywa upya nia zetu.
Wakolosai 3:10 " mkivaa utu mpya, unaofanya upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba." kuna uwezekano wa kuwa na ufahamu sawasawa na Mungu kwa sababu tumeumbiwa.


HITIMISHO:
1.Watu wa Mungu neema hii ya wokovu tuliyopewa bure imetupasa kusimama kwayo na tuishi tukitambua kwamba;
-Ni lazima fahamu zetu zibadilishwe.( Warumi 8;29) Tumeokolewa ili kuwa mfano wa Kristo.
-Kufanana na Kristo kunahitaji utayari wa kubadilika ufahamu siku hadi siku.(Waefeso 4;13).
-Mungu alikusudia mwanadamu ajae ufahamu wa Kimungu ndani yake ( sura na mfano wa Mungu)- Mwanzo1;27. Mungu anataka tuone mambo jinsi anavyoona yeye.
Mungu atusaidie sana tunapotafakari Neno hili

No comments:

Post a Comment