Rose Muhando Malikia na mwimbaji wa muziki wa injili nchini akiimba stejini wakati wa uzinduzi wa Album yake siku ya jana Diamond Jubilee jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye akikata utepe wakati akizindua rasmi albam ya Rose Muhando mwimbaji wa muziki wa injili inyoitwa Shikilia Pindo la Yesu ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam jana likihudhuriwa na maelefu ya washabiki wa muziki wa injili, ambapo waimbaji mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo wakiwemo Ephraim Sekereti Kutoka Zambia, Sara K. kutoka Kenya , Upendo Kilahiro, Upendo Nkone John Lisu na wengine wengi, Katika uzinduzi huo pia Maaskofu na wachungaji kutoka Makanisa mbalimbali wamehudhuria, Katika anayeshirikiana na Mh. Ffredrick Sumaye ni Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion iliyoandaa uzinduzi huo na kushoto ni Mwimbaji Rose Muhando mwenyewe.
Askofu Mwakibolwa alipokuwa akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredric Sumaye ili kuzungumza na waalikwa na washabiki mbalimbali wa muziki wa injili. |
Mgeni rasmi Waziri Mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye ili kuzungumza na waalikwa na washabiki mbalimbali wa muziki wa Injili. |
Ephraim Sekereti Kutoka Zambia |
Sara K. kutoka Kenya |
John Lisu |
No comments:
Post a Comment