.

.

.

.

Tuesday

HIVI UNAPOOMBAGA UNATOAGA NAFASI KWA MAPENZI YA MUNGU KATIKA HICHO UNACHOOMBEA KUSIMAMA‬?

Yesu alipoenda kumwomba Baba Yake pale kwenye bustani ya Gethsemane, kuna kitu alitamani Baba Yake amfanyie lakini wakati huo huo akijua kulikuwa na mapenzi ya Baba Yake ambayo Nayo yalibidi yatimie.

Alipomwoomba Baba Yake alimwambia kile ambacho alitamani Baba Yake amfanyie lakini pia akawa yupo tayari mapenzi ya Mungu nayo yatimie hata kama ingemaanisha yale maombi yasijibiwe vil...e atakavyo Yeye.

Hili jambo Yesu alishindana nalo katika maombi kwa takribani masaa matatu.
Mashindano hayo hayakuwa yanasababishwa na ugumu wa Baba Yake kuyajibu yale maombi bali na kule Yesu kuwa tayari kuyatiisha mapenzi Yake chini ya mapenzi ya Baba Yake.

Yesu alipokuwa tayari mapenzi ya Baba Yake kutimia kule kushindana kote kukaisha akawa tayari kukinywa kile kikombe ambacho Baba Yake alitaka akinywe.

Mara nyingi katika maombi yetu tunapata shida sana kutiisha mapenzi yetu na matakwa yetu kwa mapenzi na matakwa ya Mungu wetu.

Laiti tungekubaliana na mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu hata kama kwa sasa yanaonekana magumu vipi, mashindano ambayo huwa tunakutana nayo katika maombi tusingekuwa tunakutana nayo.
Kwenye maombi mara nyingi tunakemea roho za uzito, za upinzani, za kuzuia majibu ya maombi nk wakati kwa kweli vita halisi haipo hapo.

Vita halisi katika maombi ni kufika mahali pa kusema "Lakini sivyo nitakavyo mimi bali mapenzi Yako yatimizwe. "
Hapo ndipo mashindano makuu katika maombi yalipo. Mashindano kati ya Yakobo na Mungu haikuwa kwenye uzito wa Mungu kumbariki maana alishambariki lakini ulikuwa katika tofauti ya ajenda ambazo Yakobo na Mungu walikuwa nazo.
Mungu alitaka kumbadilisha Yakobo wakati Yakobo yeye alitaka kubarikiwa zaidi.
Yakobo alishindana na Mungu kwa sababu hiyo na mpaka alipokubali kubadilishwa mashindano yaliendelea.

Yakobo hakushindana usiku kucha kwa kuwa ilihitaji usiku kucha, alishindana usiku kucha kwa kuwa ajenda yake ilikuwa tofauti na ile ya Mungu na ilihitaji usiku kucha kufanya ajenda yake ikubaliane na ile ya Mungu.

Zilipokubaliana, mashindano yaliisha. Unapoomba unaomba ajenda zako au za Mungu kwa ajili yako?

Imeandaliwa na Mchungaji Carlos Ricky Wilson Kirimbai - Facebook Page

No comments:

Post a Comment