PENUEL 2015 Maana yake mahala pa Kukutana na Mungu uso kwa uso.(Udhihilisho wa Utukufu wa Mungu) Mwanzo 32:22-30. ,Hapo mwanzo miaka ya nyuma lilikuwa Kongamano kwa majina tofauti tofauti lakini kwa mwaka huu 2015 kwenda mbele litakuwa linajulikana kama PENUEL ikiwa na maana ya kusanyiko la Kukutana na Mungu uso kwa uso katika kujifunza Neno la Mungu
Kusanyiko hili huwa linakuwa na wahubiri mbalimbaliu kutoka nchini na nje ya nchi kuleta ujumbe ambao Mungu amewaagiza kwa kusanyiko lake.
Mwaka huu watumishi waliopo kuhudumu ni Mwenyeji Apostle Onesmo Ndegi,Bishop Tengu Yoka kutoka Nairobi Kenya,Bishop Olam Mustapha kutoka Arusha Tanzania,Prof. Dr. Zacharie Mayamba Kabengele kutoka DRC,Rev. Dr. Muteba Peter kutoka Johannesburg Afrika Kusini,Aaron Timothee Tshimanga kutoka huduma ya Mji wa Tumaini Lubumbashi DRC.Karibu sana.
Ikiwa leo ni siku ya nne zikiwa zimebaki siku mbili kukamilisha Mkutano huu,Karibu upokee kwa sehemu yako kwa siku zilizo baki huwezi jua Mungu atasema nini na wewe katika siku mbili zilizo bakia.Barikiwa,
No comments:
Post a Comment