Katika Kanisa la Living Water Centre Kawe siku ya jana kulikuwa na mahafali ya 11th ya kozi inayoitwa Life Transforming kozi ambayo inakuwa ni darasa la kukulia maisha ya wokovu au darasa la utumishi katika Ufalme wa Mungu.
Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry Kawe ambaye ndio kiongozi wa kozi hiyo alikuwepo kuhudhuria mahafali hayo, ambayo kozi hiyo ilianza mwaka 2004 ikiwa na wanafunzi wachache ambapo kadri miaka inavyokwenda idadi imekuwa ikiongezeka, na tangu chuo kianze mwaka huu ni mahafali ya 11.
Mahafari hayo yalipambwa na Uimbaji,Maigizo,dance na shuhuda za kile ambacho Mungu amewatendea wanafunzi hao katika kipindi chote walichosoma.Wengi wao katika shuhuda wamesema darasa hilo limewafundisha kumtumikia Mungu zaidi
Wakitoa shukrani zao kwa Mungu na mtumishi wamesema kuwa wamefundishika vyema kwa sababu wapo tofauti sana na walivyokuwa awali kabla ya kuanza darasa na wamefanyika utu upya na kwao hadi jana wanahitimu darasa wamepata mabadiliko makubwa.
Katika risala yao walisema kuwa elimu hii ya kozi ya Life Transformation imewapa msingi na kutujenga kiroho na kimwili, pia imewapa uwezo wa kujitambua na kufikiri, kufanya mambo kwa usahihi na kufanya maamuzi thabiti juu ya maisha yao,kwa msaada wa Roho mtakatifu, aliye msaidizi wetu. Imetuwezesha kufahamu kiundani maana ya wokovu na umuhimu wa wokovu katika maisha yetu. Tumepata elimu sahihi juu ya jinsi ya kuukulia wokovu, kuwa waadilifu, kuwa na moyo wa msamaha, kujua nafasi ya kiongozi wa kiroho, nini hasa maana ya imani na utakatifu kwa ujumla wake. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kulisoma neno na kujua msaada mkubwa uliopo katika neno kwenye maisha yetu na jinsi itupasavyo kuliishi neon, Alisema msoma risala.
Katika kozi hiyo wamekuwa wakisoma na kufanya majaribio ya mitihani mara kwa mara jambo lililowasaidia kuwainua katika kukua kiroho na pia wakaahidi kuyaishi yale mema yote waliyo yapata katika darasa hilo ili kuzidi kufikia lile kusudi la Mungu aliloliweka juu yao.
Kozi hiyo huwa inafanyika katika kanisa la Living Water Centre Ministry Makuti Kawe Dar es Salaam kila mwanzoni mwa mwaka mwezi January kwa miezi 3-4.Tangu miaka kadhaa imepita hadi mahafali hii ya mwaka 2015 kozi hiyo imesaidia watu wengi kuwa watumishi wazuri wa Mungu kutokana na masomo wanayojifunza
|
Baadhi ya wanafunzi walihitimu Life Transformation koziwakitoa shuhuda mbele ya waumini kanisani hapo wakati wa ibada |
|
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry na Mke wake Lilian Ndegi wakifuatilia shuhuda kwa umakini sana |
|
Mhitimu akitoa shuhuda mbele ya waumini kanisani hapo wakati wa ibada |
|
Baadhi ya wahitimu wa darasa hilo wakitoa shukrani zao kwa waalimu na watumishi waliohusika kuwafundisha. |
|
Wahitimu wa darasa hilo wakiimba katika kwaya yao ya pamoja |
|
Furaha kiongozi wa kwaya hiyo akiongoza nyimbo. |
|
Umati wa waumini na ndugu wa wahitimu walipohudhulia ibada hiyo kuja kuwatazama ndugu zao |
|
Apostle Onesmo Ndegi Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Ministry,Mke wake Lilian Ndegi,na wachungaji wengine waliokaa viti vya mbele wakiimba na kucheza mbele za Mungu |
|
Katika uwepo wa Bwana |
|
Mchungaji Naomi Mhamba mmoja wa waalimu wa darasa hilo |
|
Lilian Ndegi akiongoza maombi |
|
Ilikuwa furaha sana mbele za Bwana |
|
Kwaya ya The Living Waters wakihudumu katika mahafali hayo |
|
Wahitimu wakicheza na kufurahi mbele za Bwana |
|
Risala ya wahitimu ikisomwa mbele ya Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi na waumini kwa ujumla. |
|
Risala ya wahitimu ikikabidhiwa kwa Kiongozi wa Kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi na wachungaji wengine |
|
Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center Apostle Onesmo Ndegi akijibu risala ya wahitimu |
|
Pia mahafali hayo yalikwenda sambamba na ugawaji wa vyeti kwa wahitimu hao |
|
ugawaji wa vyeti kwa wahitimu hao |
|
Mmoja wa wahitimu hao alipokuwa akizungumza juu ya wao kama darasa la Life Transformation kozi juu ya zawadi walizo nazo kwa watumishi walio husika katika kuwatumikia na kuwaundisha |
|
zawadi zikigawiwa kwa watumishi na waalimu wa darasa hilo. |
|
Baadhi ya zawadi za vifaa vya usafi zilizo wasilishwa na wahitimu wa darasa hilo katika mahali hayo |
|
Lilian Ndegi mmoja mwa waalimu wa darasa hilo alipokuwa akiongea na kuwahisi wahitimu hao juu ya maisha yao ya Mungu baada ya kumaliza darasa |
|
Picha ya pamoja kati ya wanafunzi na watumishi wa Mungu walihusika katika kipindi chote cha darasa Life Transformation kozi |
|
Picha ya pamoja kati ya wanafunzi na watumishi wa Mungu walihusika katika kipindi chote cha darasa Life Transformation kozi |
No comments:
Post a Comment