.

.

.

.

Monday

Mkuu wa Wilaya Kinondoni mpya Paul Makonda Awasihi wakriso kusimama katika nafasi zao

Paul Makonda Mkuu mpya wa Wilaya Kinondoni siku ya jana amewasihi Wakristo kusimama katika nafasi zao,aliyasema hayo alipokaribishwa kusalimia huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru Mungu kwa uteuzi huo wa kuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kinondoni aliongozana na Mke wake katika Ibada hiyo Katika Kanisa la Living Water Center Kawe chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi ndio kanisa lililomlea tangu anasoma Chuo kabla ya kuingia kwenye siasa mpaka kupata uteuzi huo.

Alisema anamshukuru Mungu kwa nafasi ya uteuzi huo kwa kusema jinsi Kinondoni inavyoongoza kuwa Wilaya kubwa na inayoongoza kwa miradi mbalimbali ya Kiserikali na mambo mengi ikiwepo mambo mabaya kama machangudoa,vibaka,madawa ya kulevya na uharibifu mwingi ila kama wakristo tukiweza kusimama na katika zamu zetu na kushughulika  na hali hizo zitaweza kuondoka na tukawa na wilaya yenye matukio yenye kumpa Mungu Utukufu Alisema Mkuu huyo wa Wilaya 

Paul Makonda Mkuu mpya wa Wilaya Kinondoni

Mkuu wa Wilaya  Kinondoni mpya Paul Makonda na mke wake
Washirika wa Kanisa hilo walipomuombea kwa kumuwekea mikono  Mkuu huyo wa Wilaya  Kinondoni  

No comments:

Post a Comment