Alipoondoka Sudan alipitia Italy ambako alikutana na Papa Francis |
Rosa Parks alisifika na kutazamwa kuwa ushujaa wa harakati za haki za kiraia nchini Marekani alipokataa kuondokea mwanamme mzungu kitini wakiwa ndani ya gari huko Alabama.
Hatimaye Nutter alimkabidhi Meriam mfano wa ‘kengele ya uhuru,’ ishara ya uhuru wa Marekani. Aidha, kwa mujibu wa msemaji wa Vertican, Bi Meriam akiwa Rome alikutana na papa ‘aliyemshukuru kwa kuwa imara katika Imani yake.”
Safari ya Bi Meriam ilifikia kikomo New Hampshire kwani alikuwa anasubiriwa kwa hamu na ghamu na jamaa na wafuasi wake katika uwanja wa ndege.
Meriam aliponea kifo baada ya mahakama kubatilisha uamuzi wa kumnyonga kwa kuasi dini |
Mumewe Bi Meriam, Daniel Wani, pia ni muumini wa kikiristo na pia ni mzaliwa wa Sudan kusini lakini ana uraia wa kimerakani.
Kwa mujibu wa mwanahabari wa BBC aliyeshuhudia tukio hilo, Meriam alikaribishwa na halaiki ya watu, wengine wao wakiimbia “Marekani iishi milele.”
Aidha mwanahabari wetu alituarifu kuwa mume wa Bi Meriam alitoa hotuba fupi na kushukuru serikali ya Marekani na maseneta wa New Hampshire kwa kumpigania na kwa kufanya mipango ya kumpa mke wake hifadhi. Pia alishukuru watu wa Sudan kwa usaidizi wao.
Familia ya Meriam inakusudia kuishi New Hampshire kwani jamaa wa mume wake wako huko.

SOURCE:BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment