.

.

.

.

Wednesday

Tamasha La Bomby Johnson Lafana ndani ya VCCT

Mwanamuziki Wa Injili ambaye ameshirikiana na Wanamuziki wengine katika albam zao kama Vile Miriam Lukindo wa Mauki, Upendo Nkone, John Lisu, Amani Kapama na wengine wengi anayejulikana kwa jina la Bomby Johnson jioni ya siku ya leo amefanya Tamasha la Kusifu na Kuabudu lenye jina la “Worship In The Terbanacle” yaani “Ibada Katika Hema La Kukutania”. Katika Tamasha hilo lililoanza majira ya saa 9 na nusu alasiri lilimalizika majira ya saa 1:45 Usiku ambapo mpaka muda huo bado watu walikuwa katika Ukumbi wa VCCT.

Katika Ibada hiyo ya Kusifu na Kuabudu Mwanamuziki Bomby Johnson alisindikizwa na wanamuziki John Lisu, Meshack Kutoka VCCT, David Abel, Paul Clement, Rivers Of Joy International, pamoja na mpiga saxophone maarufu Mise Anael.


 

















No comments:

Post a Comment