.

.

.

.

Tuesday

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI LUSAKA KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KWENYE SHEREHE ZA KULA KIAPO RAIS WA ZAMBIA EDGAR LUNGU

Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe Grace Mujuma akiwa na Balozi wa Zambia nchini Tanzania Mhe Judith  Kapijimpanga wakifurahia wakati ndege iliyomchukua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ilipotua katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia, jana Jumatatu Septemba 12, 2016  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu leo Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea shada la maua  mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu  Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Michezo na Maendeleo ya Watoto Mhe. Agnes Musunga   akipokea heshima mara baada ya kutua  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka, Zambia,  tayari kwa kumuwakilisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwenye sherehe za kuapishwa rais wa sita wa nchi hiyo Mhe. Edgar Lungu leo Jumanne Septemba 13, 2016 katika uwanja wa Mashujaa jijini Lusaka

No comments:

Post a Comment