.

.

.

.

Saturday

Waimbaji Kutoka Uingereza Atua Kunogesha Tamasha La Pasaka

jbfvkjv
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi
Kelechi, akipokea ua kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Msama Promotions.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi
Kelechi akisalimiana na Msama katika uwanja wa ndege baada ya kuwasili. 


Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza Ifeanyi
Kelechi akiimba mbele ya wandishi wa habari.

Miller Luwoye akizungumza na waandishi wa habari.

Anthonia Nwafor
Mwandaaji wa Tamasha la Pasaka Bwana Msama akizungumza na waandishi wa habari.

Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama (wa pili kulia) akiwa na waimbaji kutoka Uingereza.
Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Uingereza, Ifeanyi Kelechi, ametua nchini kwa ajili ya kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.Kelechi, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jana saa mbili asubuhi kwa ndege ya Shirika la Qatar, akiongozana na wenzake wanne.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Kelechi alisema lengo la ujio wake ni kuhakikisha tamasha hilo linanoga kuliko yaliyowahi kufanyika, ndio maana amekuja na jopo la waimbaji watano.“Namshukuru Mungu kutufikisha salama, nimefurahi sana kufika Tanzania kwa mara ya kwanza, hasa kuja kuimba kwenye tamasha kubwa kama hili, ambalo naamini litakuwa chachu ya kumfanya kila mtu kuvutiwa nalo,”alisema.Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama, alisema kuzidi kumiminika kwa waimbaji, kunaashiria tamasha hilo litanoga zaidi.

“Waimbaji wetu wameshaanza kuwasili nchini na kesho waliobakia watawasili…Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa, tunaisubiria siku hiyo tu,” alisema Msama.Tayari muimbaji Faustine Munishi ‘Malebo’ mtanzania anayeishi nchini Kenya tayari kawasili tangu juzi huku Ephraim Sekeleti wa Zambia, Rebecca Malope na Solly Mahlangu ‘Obrigado’ kutoka Afrika Kusini watafuata. Mbali na waimbaji hao kutoka nje, watakuwepo pia wakali wa hapa nchini wakiwamo Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro
na wengineo.

Source:fullshangweblog

No comments:

Post a Comment