.

.

.

.

Monday

Mchungaji: Liombeeni Bunge lijadili mambo ya wananchi.

Watanzania wametakiwa kupiga magoti kuliombea Bunge ambalo vikao vyake vimekuwa vikitawaliwa na maneno ya kukashifiana ambayo hayana utukufu wa Mungu na kuwaweka njia panda wananchi.

Rai hiyo ilitolewa na Mchungaji Kiongozi wa kanisa la FPCT Nkuhungu, mkoani hapa, Johnson Mpili, alipokuwa akihubiri kwenye ibada ya Pasaka jana.

Alisema Watanzania wana kila sababu ya kuliombea Bunge hilo kutokana na malumbano na mivutano ambayo imekuwa kero kwa wananchi waliowachagua wabunge kuwawakilisha na  kutatua matatizo yanayowakabili.

Alisema wabunge hivi sasa hakuna wanacho zungumza chenye maslahi mapana ya wananchi, zaidi ya malumbano, kejeli na matusi, mambo ambayo hawakutumwa na wananchi waliowapigia kura.

“Wabunge wamegeuza jengo hilo kama kijiwe cha kutoleana maneno ya kukashifiana bila kujali thamani waliyonayo kama wabunge waliochaguliwa na wananchi walala hoi,” alisema.

Pia aliwataka Watanzania kumuomba Mungu ili wabunge watakaochaguliwa katika uchaguzi wa mwaka huu wawe wenye hofu na Mungu na watakaoweka masilahi ya wapiga kura wao mbele.

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Endtime Harvest, Dk.  Eliah Mauza katika mahubiri yake, aliwataka Watanzania kudumisha amani, upendo na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment