Ukitaja
Harry Porter watu wengi wanajua kuhusu Movies na Vitabu maarufu sana
vilivyoandikwa na Mwandishi maarufu wa uingereza J.K Rowling ambaye
amefanikiwa sana kupitia kazi zake za uandishi.Lakini kitu ambacho watu
wengi
hawajui kuhusu J.K Rowlings ni mambo aliyoyapitia katika maisha yake
hadi kufika hapo alipo sasa hivi.
Mwaka 1990 ndio kwa mara ya
kwanza
alipata wazo la kuandika kuhusu Harry Porter na wazo hili lilikamilika
zaidi alipokuwa safarini kwenye treni akitokea Manchester kwenda
London.Mara
baada ya kuona ni wazo linaloweza kubadilisha maisha yake aliamua
kulifanyia kazi kwa haraka na akaanza kuandika kwa bidii sana.Hata
hivyo,mwaka
huohuo mama yake alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Miaka
miwili baadaye alihamia ureno ambako alianza
kuwa mwalimu wa lugha ya kiingereza ambako pia alikutana na mwanaume
ambaye alimuoa na alipata mtoto wa kike.Mwaka mmoja baadaye (1993)
aliachwa na
akaamua kurudi uingereza kwenye mji wa Edinburg wakati huo alikuwa
tayari ameandika sura 3 za kitabu chake cha Harry Porter.Aliporudi
Uingereza maisha
yalikuwa magumu saidi na alijiona kama vile ndoto yake ya kuandika
kitabu imeshakufa kwani alikuwa hana kazi,ameachwa na ana mtoto wa
kumtunza.Ghafla
akajikuta yuko kwenye msongo mkubwa wa mawazo(stress) na
mfadhaiko(depression) mkubwa sana.Hivyo aliamua kujiorodhesha katika
mpango wa
serikali ambao unasaidia watu maskini(Government welfare program).
Mwaka
1995 alijaribu kupeleka kitabu chake kwa
wachapishaji zaidi ya 12 na wote walikataa kuchapisha kitabu chake
lakini mwaka mmoja baadaye kampuni moja ndogo(Bloomsbury) sana ikakubali
na
kumchapishia kopi 1000 tu na huku 500 zikigawiwa kwenye maktaba na
alilipwa paundi 1500 za utangulizi.Miaka miwili baadae(1997 na 1998)
kitabu chake
kikashinda tuzo toka Nestle Smarties na British Book Award kama kitabu
bora cha watoto cha mwaka.Baada ya hapo Rowling ameuza zaidi ya kopi
milioni
400 ya kitabu chake na ndio anachukuliwa kama mwandishi mwenye mafanikio
zaidi nchini Uingereza.
Jambo
kubwa la kulijua hapa ni kuwa
bila kujali una ndoto ya kufanya nini ama unataka kukamilisha jambo gani
katika maisha yako ni lazima utapitia nyakati ngumu na zenye kukatisha
tamaa
katika maisha yako.Kuna watu wengi sana ambao wameshindwa kufanikiwa
katika maisha yao sio kwa sababu hawana uwezo ama kipaji cha kuwafanya
wafanikiwe
lakini kwa sababu wameshindwa kuendelea mbele katika kufuatilia malengo
yao hasa baada ya kushindwa mara kadhaa baada ya kujaribu.Kama kweli
unataka
kufanikiwa kwa kiwango cha juu sana lazima uwe mtu ambaye hauko tayari
kushindwa katika jambo lolote lile kwenye maisha yako.
Kuna
watu
wengi sana wanaokufa na vipaji vyao,wanakufa na uwezo wao ambao
ungeweza kuwasaidia sana kubadilisha maisha yao.Nawe najua unasoma
Makala hii kwa
sababu unatamani kufanikiwa kufikia kilele cha ndoto yako,lakini ukweli
ni kuwa kama hautakuwa tayari kuchukua hatua madhubuti basi itakuwa
ngumu sana
kwako kufanikiwa.Mafanikio huanza na uamuzi thabiti unaotoka ndani ya
moyo wako kuwa kweli unataka kupiga hatua katika maisha yako.Uamuzi huu
hakuna
mtu anayeweza kukufanyia isipokuwa wewe mwenyewe,ni lazima ufike sehemu
uufanye.
Mara
nyingi uamuzi wa namna hii unaweza kutokana na
kutaka kuepuka maumivu(To avoid pain) au kutokana na kutamani kupata
raha (to seek pleasure).Historia za wengi waliofanikiwa ni lazima
walihusisha
kitu kimojawapo kati ya viwili.kuna watu ambao walipitia wakati mgumu
sana katika maisha yao na kwa sababu hiyo walijikuta wamefika sehemu
wamechukia
maisha ya umaskini na wakakata shauri ndani ya mioyo yao la kutaka
kuanza safari mpya ya mafanikio,kwa maneno mengine hawataki kabisa aidha
wao au
ndugu ama watoto wao wapitie hali ya mateso ambayo wao wamepitia.Kwa
upande mwingine kuna watu ambao waliishi maisha ya kawaida tu lakini
wameona
jinsi wengine ambavyo wamefanikiwa katika maisha yao na wao wametamani
kuishi kama hao wengine.Katika maisha hakuna mtu anayefanikiwa kwa
bahati
mbaya,hata wewe kama kweli unataka kufanikiwa ni lazima uamue kuanzia
leo.
Swali
la msingi ambalo ni muhimu kujiuliza ni
kuwa;hivi kwa nini watu wengi hawafanikiwa katika maisha na wachache
ndio huwa wanafanikiwa?Ziko sababu kuu 4 ambazo zinawafanya watu
washindwe
kufanikiwa katika maisha yao:
• HOFU YA KUFANYA JAMBO JIPYA
Tafiti
za kisaikolojia zinaonyesha kuwa kila mtu huwa hapendi kuondolewa
kutoka mahali alipopazoea(comfort zone).Hii ndio maana kuna watu
kanisani kila jumapili watakaa upande huohuo na wengine kiti kilekile na
wakikuta kuna mtu amekaa huwa wanaona kama vile wamekalia kiti
chao.Hata
nyumbani ukichunguza vizuri kuna watu huwa wanakaa kochi hilohilo ama
kiti hichohicho wakati wa kula hata kama hajawahi kupangiwa kuwa akae
hapo.Ndivyo ilivyo katika maisha ya kawaida watu wengi huwa hawapendi
kubadilika.Kuna watu kila wakienda na kurudi kazini wanapita njia ileile
kwa
miaka nenda rudi,hata kama kuna njia nyingine hawajawahi kujaribu
kabisa.
Hebu
jichunguze kitu ambacho unakifanya kwa sasa hivi
umekuwa ukikifanya kwa muda gani na kwa nini haujabadilisha hadi leo.Leo
fikiria kuna kitu gani kipya ambacho unaweza kuanza kukifanya kwenye
maisha
yako?Usikubali mwaka huu uiishe kabla haujaanza kufanya kitu kipya
tofuati na unachofanya sasa hivi.Kumbuka kuwa Henry Ford alisema ““If
you always do what you’ve always done, you’ll always get what you’ve
always got.”(Ukiendelea kufanya mambo yaleyale ambayo
umekuwa ukifanya sikuzote basi utapata matokeo yaleyale ambayo umekuwa
ukiyapata)
• HOFU YA KUFELI/KUSHINDWA
Sababu
nyingine inayowafanya watu washindwe kufanikiwa ni ile hofu ya
kushindwa.Kuna watu wengi sana ambao wameogopa kufanya jambo fulani
kwenye maisha kwa sababu ya hofu ya kuwa watashindwa.Mara nyingi,wazo la
kwanza ambalo watu huwajia katika akili yao inapofika kufanya jambo
fulani
huwa ni “itakuwaje nisipofanikiwa”.Kuna watu wanaogopa kufanya biashara
kwa sababu ya kuwa na hofu ya kupata hasara,kuna watu wanaogopa
kuomba kazi mahali kwa sababu ya hofu ya kukataliwa,kuna watu wanaogopa
kuanza kulima kwa sababu ya hofu ya kupata hasara. Mtu mmoja mwenye
hekima
alisema — “Everything you want is on the other side of fear”(Kila kitu ambacho kwa sasa hauna na unakitaka,kipo
upande wa pili ukishaivuka hofu).Mafanikio yako yamejificha nyuma ya hofu inayokukabili.
Kama
kweli unataka kufanikiwa katika maisha yako ni
lazima uanze kuishi katika namna ambayo hofu ya kufeli haina nafasi.hebu
jiulize leo,kuna mambo mangapi ambayo unatamani kuyafanya lakini
kinachokuzuia ni hofu ya kushindwa?Leo anza kuishinda hofu hiyo na anza
kuchukua hatua mara moja.Kuanzia leo ningekushauri kutumia kanuni hii
aliyowahi kuisema Jack Carnfield aliposema –‘'Don't worry about
failures, worry about the chances you miss when you don’t even
try”(Usiogope kufeli bali ogopa mafanikio ambayo unaweza kuyakosa
uanpoogopa kujaribu).
• KUTUMIA VISINGIZIO VYA KUTOKUWEZEKANA
Jambo
la tatu linalosababisha watu wafeli katika maisha yao ni ile hali ya
kutumia visingizio walivyonavyo katika maisha yao.Wengine
watatumia visingizio vya kutokusoma/kutokuwa na elimu ya kutosha,wengine
watatoa visingizio vya hali mbaya ya uchumi,wengine watatoa visingizio
vya
familia walizotoka n.k./UKweli ni kuwa wakatai wowote ule ukitaka kupata
visingizio vya kutofanya jambo fulani basi utavipata vingi sana,ila
kama
kweli unataka kufanikiwa ni lazima uamue kutokuwa mtu wa visingizio
kabisa katika maisha yako. Jim Rohn aliwahi kusema 'If you
really want to do something, you'll find a way. If you don't, you'll find an
excuse”(Kama kweli uantaka utatafuta namna ya kupata,ila kama hautaki basi utatafuta visingizio)
Kuna
mambo mengi leo
ukiulizwa kwa nini huyafanyi utajikuta unatoa visingizio,kumbuka kuwa
kila unapotoa visingizio basi unapoteza uwezo wako wa kutatua changamoto
inayokukabili.Kuanzia leo amua kuwa mtu ambaye hautoi visingizio na
badala yake uwe mtu wa kuchukua hatua.Watu wanaotoa visingizio kila siku
watamlaumu mzazi,ndugu ama rafiki.Amua kuachana na visingizio kuanzia
leo-Anza hivyo biashara,anza kilimo,chukua hatua.
• KUJILINGANISHA NA WENGINE
Jambo
la nne linalowasababisha watu wafeli kabisa ni ile hali ya
kujilinganisha na wengine.Ni vyema nianze kwa kukuambia kuwa wewe
umeumbwa kuwa wa tofauti,hakuna mtu yoyote yule ambaye unafanana naye
kabisa.Mungu alipokuumba aliweka ndani yakio uwezo wa kipekee na uwezo
wenye
nguvu sana wa kubadilisha maisha yako kabisa.Usifanye kosa hata siku
moja kujilinganisha na wengine.Kuna watu wengi sana waliumbwa na uwezo
mkubwa
kama tembo ila kwa sababu wamekuwa wakiishi na watu wenye uwezo mdogo
kama sungura wamejikuta wanaishi maisha ya kawaida sana.
Hata
kama
kila mtu anaishi maishi ya kawaida,ya chini,ya kushindwa-Kumbuka wewe
haujauumbwa uishi hivyo.Wewe umeumbwa kuwa mshindi,wewe umeumbwa
kufanikiwa,wewe umeumbwa kuinuka hadi juu.Usiangalie wengine wanaoishi
kawaida nawe ukajiweka kuwa mmoja wao,usiangalie kiwango cha maisha cha
familia
yako,usiangalie kiwango cha maisha cha majirani na ndugu
zako-HAPANA.Wewe nafasi yako sio hapo,wewe nafasi yako ni juu
zaidi.Inawezekana leo unaishi
maisha ya taabu na yenye kukatisha tamaa,unachotakiwa kujua ni kuwa hayo
ni maisha ya mpito na unaweza kuyabadilisha kama ukiamua.
Kama
kweli
umesshafanya maamuzi ya kuamua kufanikiwa katika maisha yakobasi ni
vyema ukajua namna ya kuanza kuishi kuanzia leo ili uanze safari yako ya
mafanikio.Ziko njia tatu unazoweza kuanza kuzitumia kuanzia leo ili
ujiunge na wale ambao wanafanikiwa kila siku:
• AMINI KWAMBA INAWEZEKANA.
Jambo
la kwanza kabisa katika safari yako ya mafanikio ni uwezo wako wa
kuamini kuwa unalotaka kufanikiwa linawezekana.Watu wengi sana
huwa wanafeli hata kabla hawajajaribu kwa sababu kabla
hawajaanza,utasikia-“Hili haliwezekani”.Kama kweli unataka kufanikiwa ni
lazima uwe
na imani kuwa inawezekana;ndio-Inawezekana kuwa tajiri,inawezekana
kupona,inawezekana kufaulu mitihani,inawezekana kuanzisha biashara n.k
Mara
nyingi
hatua hii huwa ni ngumu sana kwa muda mrefu tunakuwa tumeaminishwa kuwa
kile tunachokitaka hakiwezekani.Imani hizi hutokana na maneno
tuliyoambiwa na wazazi wetu,walimu wetu,marafiki ama mazingira ambayo
tumekulia.Kutokuwezekana kwa jambo mara nyingi ni fikra ambayo
imejengeka ndani
kabisa ya ubongo wetu na hakuna namna tunaweza kuitoa bila kuamua na
kutumia mikakati madhubuti.
Ili
fikra ya kutokuwezekana iondoke
kabisa katika akili yetu tutahitaji kujiambia wenyewe mara nyingi zaidi
kuwa inawezekana kuliko mara ambazo tumeshawahi kusikia kuwa
haiwezekani.Hii
ndio maana kuna wakati utatakiwa kuchukua malengo yako na ukae peke yako
mahali na uyasome na useme kwa sauti-“Haya yote
yanawezekana”.Kila wakati wazo la kuwa utafeli,utapata hasara au wazo la
haiwezekani linapokuja ndani yako basi jiambie kwa sauti kuwa
inawezekana.
Je,kuna jambo lolote ambalo ulikuwa unalitamani kulifanya ila unakwa unaona kama vile
halitawezekana?.Leo lichukue jambo na useme-Hili nalo linawezekana.
• PATA MAARIFA UNAYOHITAJI
Ili
uweze
kufanikiwa katika malengo yako ni lazima ujijenge katika maarifa muhimu
yanayotakiwa kukusaidia kutimiza malengo yako.Kama unataka kufanya
biashara basi hakikisha kuwa unapata ujuzi wa kutosha kuhusiana na
biashara unayotaka kufanya.Uwe mtu ambaye uko tayari kila wakati
kugharamia maarifa
ambayo yanaweza kuwa msaada kwako katika kutimiza malengo yako.
Uwe
tayari kutumia pesa yako kwa ajili ya kununua
vitabu,CDs,DVDs n.k ili kujenga uwezo wako wa kufuatilia na kutimiza
malengo yako.Hakikisha kuwa kila siku haipiti bila kujifunza kitu kipya
kinachochangia katika kukusaidia kutimiza malengo yako.Kumbuka kuwa
kiwango cha maarifa uliyonayo ndicho kinatengeneza kiwango cha mafanikio
utakayopata katika malengo uliyojiwekea.Weka bajeti yako maalumu ya
kununua vitu ambavyo vinakusaidia.Pia jilazimishe kutumia muda wako
katika
kujijenga zaidi na sio katika kujiburudisha.Kama wewe unaweza kushinda
kwenye televisheni masaa mawili ama kuchart kwenye facebook ama watsapp
lisaa
lizima lakini huwezi kutumia hata nusu saa kujisomea kitabu basi ujue
bado uko mbali na mafanikio.Hebu jaribu sasa kuweka mkakati wa namna
ambavyo
utakuwa unaongeza maarifa kila siku ili kufanikisha malengo yako.
• ANZA LEO,ANZA SASA
Kati
ya
vitu hatari sana kuelekea katika mafanikio yako ni ile hali ya
kughairisha mambo kila wakati.Kuna watu wengi sana wakati mwaka huu
unaanza
walijiwekea mipango mingi sana lakini hadi leo hawajaanza hata mpango
mmoja kati ya hiyo(sina uhakika kama na wewe ni mmoja wao).Tatizo la
kughairisha
kuanza limewafanya watu wengi sana washindwe kufanikiwa katika maisha
yao.
Watu
wengi ukiwauliza sababu za wao kutoanza yale
mambo ambayo wanayatamani kuyafanya watakupa visingizio vya kuwa
mazingira hayaruhusu,bado hawajapata mtaji,bado wanasubiri mtu wa
kuwasapoti n.k.kama
kweli unataka kufanikwia katika maisha yako ni lazime uwe mtu ambaye uko
tayari kuanza pale ulipo kwa kutumia kile ulichonacho.Kila lengo
ulilonalo
lina hatua ambayo unaweza kuichukua kwa sasa.
Usiwe
mtu ambaye kila wakati unasubiri kila kitu kiwe sawa ili uanze kuchukua
hatua,hapana-Martin Luther King Jr aliwahi kusema-“Faith is taking the
first step when you don’t see the whole staircase”(Imani ni
kuanza kupanda ngazi ya kwanza hata kama hauoni mwisho wa ngazi
unayopanda).Acha kuwa wale watu waanitwa “nitaanza
kesho”(Mr/Mrs.Tommorow)-Wewe kila siku ukikutana na wenzako wakikuuliza
kuhusu malengo yako,kazi yako ni kusema nitaanza kesho.Jitahidi uanze
kutekeleza wazo lako kuanzia leo.
Kama ujumbe huu umekuwa na manufaa kwako,basi tafadhali utume kwa wengine ili waweze
kufaidika nao pia.
Siku
zote kumbuka kuwa mafanikio yanapatika kwa wale watu ambao wako tayari
kuzingatia mambo hayo hapo
juu.Kama ungependa kupata mafundisho ya namna hii kila siku basi unaweza
kutembelea na kulike ukurasa wangu wa facebook(Joel Nanauka) au
instagram
(joel_nanauka) na utapata mafundisho ya kukusaidia kuifanikisha ndoto
yako kila siku.Pia unaweza kujiunga na madarasa kwa njia ya WATSAPP kwa
kutuma
neno “NDOTO YANGU” ikifuatiwa na jina lako kamili kwenda 0655 720197 na utaunganishwa na hakuna gharama yoyote ile utakayotozwa.
Kama
ungependa
kupata ushauri zaidi kuhusu namna ya kutimiza malengo yako ama
ungependa kunieleza Makala hii ilivyokusaidia,tafadhali tuwasiliane kwa
barua
pepe(jnanauka@gmail.com ama kwa simu 0743 868507 au tembelea tovuti yangu www.JoelNanauka.Com).
See
You At The Top
Joel Nanauka
Source:www.JoelNanauka.Com).
No comments:
Post a Comment