Wapendwa, kama watoto
wa Mungu, tusikubali kuyumbishwayumbishwa ama kubabaishwa na chochote
kila katika maisha haya. Tuelewe ya kuwa uzima wetu na maisha yetu vimo
ndani ya Mungu – Yes – ndani ya Mungu Mwenye Enzi yote Baba wa Bwana
wetu Yesu Kristo na tunaishi kwa uweza wake, Mtume Paulo alikuwa na
mengi ya kusema kuhusu hili, ngoja niorodheshe japo machache.
Paulo alisema ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. (Matendo 17:28) Na mahali pengine akasema tulikufa na sasa uhai wetu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu (Wakolosai 3:3)
Na kama hiyo haitoshi tumekumbushwa na Mtume Paulo mara kadhaa ya kuwa
baada ya Kristo Yesu kutufia pale msalabani na kutupatanisha na Baba
basi hii miili yetu inafanyika Hekalu la Roho Mtakatifu
tunapomwamini
Yesu (1 Wakorintho 6:19). Mtume Paulo pia alifikia kusema hivi:
20
Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali
Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao
katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake
kwa ajili yangu. - Wagalatia 2:20 SUV
Tumeungamanishwa na Mungu na kuwa roho moja naye...we are no longer separated from God! Wow!
17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. – 1 Wakorintho 6:17 SUV
Nimekakumbuka kale kawimbo ketu kazuri... “Siyo mimi ninayeishi bali Kristo ndani yangu,...”
Natamani
tunapokaimbaga tuimbe tukitafakari kweli hii ya kwamba Mungu wa Milele
yote, Mungu Mwenye Enzi na Mamlaka yote, Muumba wa Mbingu na Nchi na
vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo,
pamoja na Kristo Yesu mwenyewe wameweka makao ndani yetu - tusiishie
kuimba kimazoeamazoea tu.
Wapendwa yaani if we only knew the Treasure we have in these earthen vessels....if we only knew...
Mpendwa
mtoto wa Mungu, amini na uelewe ya kuwa upo ndani ya Kristo na Yeye
yupo ndani yako muda wote, 24/7, mithili ya Mzabibu na matawi yake, hata
kama hisia zako zinagoma au mazingira yako hayaonekani kuwa
hivyo....Hisia zetu hubadilikabadilika, mazingira yetu nayo vivyo hivyo,
lakini lile asemalo Mungu limethibitika milele hivyo halibadiliki.
Hivyo
simama imara katika ufahamu huo na uyakabili maisha ukijua aliye ndani
yako ni Mkuu kuliko aliye katika Dunia na wewe kama mtoto wake
uliyezaliwa kwa Mbegu isiyoharibika ya Neno lake, amekushirikisha asili
yake ya Kiungu ambayo inakupa hekima, maarifa, ufahamu na yote
unayohitaji ili kuweza kuyakabili, kuyamudu na kuyaboresha maisha yako
na ya wanaokuzunguka kwa utukufu wa Mungu.
Mpendwa, unayaweza mambo yote katika Kristo Yesu akutiaye nguvu! Chukua hatua…With Christ you can do all things!
Somo na Patrick Kamera
No comments:
Post a Comment