“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa
vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu
akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.” (MWA. 1:1-3 SUV).
Hapo mwanzo kabisa
Mungu alipoziumba mbingu na nchi kila alichokiumba kilikuwa kamili
pasipo kasoro.
Kuna kitu kilitokea ambacho bibilia imeamua kunyamaza
kimya ambacho kilisababisha hizo mbingu na nchi zilizoumbwa katika hali
ya ukamilifu pasipo kasoro ziwe ukiwa na utupu, na hiyo hali ya ukiwa na
utupu ilifanywa mbaya zaidi na hali ya giza lililofunika uso wa vilindi
vya maji.
Pamoja na uwepo wa Mungu juu ya uso wa maji, hamna ambacho
kingeweza kufanyika alimradi giza lilikuwepo juu ya uso wa vilindi vya
maji. Mungu alipotaka kushughulika na hali ya utupu na ukiwa kitu cha
kwanza ambacho ilibidi ashughulike nacho ni hilo giza ambalo lilikuwa
linaipa nguvu huo ukiwa na utupu. Mungu akasema iwe nuru
Kutoka Kwa Pastor Carlos Kirimbai.
No comments:
Post a Comment