.

.

.

.

Tuesday

Mchungaji Carlos Ricky Wilson Kirimbai

Huku kwenye mitandao ya jamii nako kuna haja kubwa sana ya kuzijaribu roho na sio tu kubugia kila kinachoachiliwa kwenye social media.

Mafundisho mengi humu ni uncensored, yatokanayo na roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani.
Hamna kitu hatari kama kujiona unajua wakati bado hujajua ikupasavyo kujua.

“Mtu akidhani ya kuwa anajua neno, hajui neno lo lote bado, kama impasavyo kujua.” (1 KOR. 8:2 SUV).
Wengi wamejipachika ualimu, uchungaji, unabii na utume humu na wanamwaga mashule sumu sana na kwa kuwa social medianites ndo wengi wanashinda humu na hawasomi neno kiviile ngumu sana kugundua matango pori hasa yale ambayo yamechomekewa chachu kidogo.

Wito wangu kwa social medianites ni pata muda pia wa kutulia na neno la Mungu maana namna pekee ya kuijua siyo ni kujua vizuri ndiyo.

Nikiangalia siku za usoni, wengi sana watapotoshwa na mafundisho uncensored yanayomwagwa humu.
Tukumbushane maneno ya Yakobo Mtume:
“Ndugu zangu, msiwe waalimu wengi, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi. Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.”
(YAK. 3:1-2 SUV).

Tukumbushane pia maneno ya Mtume Paulo kwa mwanae Timotheo.
“Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.” (2 TIM. 4:3-4 SUV).

Na Mtume Petro naye alikuwa na haya yakusema:
“Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii.” (2 PET. 2:1-3 SUV).

Hatari inazidi kuongezeka siku hizi za mwisho kwa sababu ya nguvu ya social media kufikia watu wengi kwa mara moja tena kwa haraka.

Imeandaliwa na Mchungaji Carlos Ricky Wilson Kirimbai - Facebook Page

No comments:

Post a Comment