Siku kadhaa zimepita tangu washindi mbalimbali wa tuzo za AMVCA 2016 zilizofanyika Lagos nchini Nigeria watangazwe baada ya mchujo wa wasaani wengi kwa vipengele mbalimbali,kwa upande wa Tanzania Afrika Mashariki tuliwakilishwa vyema na Rich au Single Mtambalike na Movie yake ya Kitendawili na Lulu maarufu kama Elizabeth Michael kwa movie yake ya Mapenzi ya Mungu.
Baada ya ushindi huo Lulu ameona ni vyema kurudi madhabahuni kumshukuru Mungu kwa ushindi huo,siku ya jana katika kanisa la Living Water Centre Ministry Kawe kwa Apostle Onesmo Ndegi anapolelewa kiroho baada ya kuwa amempa Bwana Yesu maisha yake au kuokoka ndipo mahala alipokuwa akimshukuru Mungu.
Akiongea alisema anamshukuru Mungu maana alimpa ujasiri wa kwenda kwenye tuzo hizo huku akijua ana rudi na tuzo!
|
Apostle Onesmo Ndegi akieleza ambavyo Lulu alikuja kumuaga wakati anakwenda Nigeria kwenye tuzo za AMVCA 2016 na akamuombea mwisho akarudi na ushindi |
|
Elizabeth Michael kushoto maarufu kama Lulu akieleza kile Mungu amemtendea |
|
Elizabeth Michael akiwa na Lilian Mke wa Apostle Ndegi mmoja wa waalimu wanaomsaidia katika masomo ya ushirika wake na Mungu |
source:gospelhabari.blogspot.com
No comments:
Post a Comment