.

.

.

.

Thursday

Mcheni Mungu na Kuzishika Amri zake

“Dunia inaomboleza,inazimia,ulimwengu unadhoofika,unazimia,watu wakuu wa dunia wanadhoofika.tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa,kwa maana wameziasi sheria,wameibadili amri.wamelivunja agano la milele.Ndiyo sababu laana imeila dunia hii,na watu wanaoikaa wameonekana kuwa na hatia,ndiyo sababu watu wanaoikaa dunia wameteketea,watu waliosalia wakawa wachache tu” ISAYA 24:4-6

Mpendwa msomaji,tafakari sana aya hizi za utangulizi.
Unaweza kuungana na kile maandiko yanachoonyesha kuhusu hali halisi ya Dunia yetu hii leo.
Laana inaila dunia yetu hii leo kwa sababu zifuatazo

1.      “Wameziasi sheria”
2.      “Wameibadili amri”
3.      “wamelivunja agano la milele”
Hivyo katika waraka huu, mungu anahitaji kutuonyesha namna ya kuepukana na laana hiyo.ila tu nai mpaka pale tutakapogundua mambo yafuatayo:-

1.      Amri hizo za mungu ni zipi?na ni ngapi?
2.      Amri hizo za mungu ni za muhimu mpaka sasa?(kizazi hiki)
3.      Amri hizo za mungu,kila mtu anapaswa kuzijua na kuzitii? Na anwajibishwa kwa kutozifahamu au kuzivunja? Kwa hayo na yanayotokana na hayo ndiyo lengo la waraka huu.mungu akubariki uanaposoma Neno Lake.

AMRI ZA MUNGU NI ZIPI NANI NGAPI?

1.      Usiwe na miungu mingine ila mimi.KUTOKA 20:3
2.      Usijifanyie sanamu ya kuchonga,wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni,wala kilicho chini duniani,wala kilich majini chini ya dunia.usivisujudie wala kuvitumikia;kwa kuwa  mimi ,BWANA Mungu wako ni Mungu mwenye wivu;nawapatiliza wana maovu ya baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne chawanichukiao,name nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu.KUTOKA 20:4-6

3.      Usilitaje bure jina la BWANA,Mungu wako maana BWANA hata mhesabia kuwa hana hatia mtu alitajae jina lake bure.KUTOKA 20:7
4.      Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.Kwa siku sita utafanya kazi zako zote, lakini siku ya saba ni Sabato kwa BWANA Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yo yote, wewe wala mwana wako au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.Kwa kuwa kwa siku sita, BWANA aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo ndani yake, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo BWANA akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.KUTUKA 20:8-11.Katika  amri ya nne,tunaagizwa  kuitunza sabato.
SABATO NI SIKU IPI?

Biblia inatuambia kuwa sabato ni siku ya saba katika wiki.biblia inasema :-
“Baada ya siku ya sabato, maria Magdalena, salome na maria mama yake yakobo walinunua manukato ili waupake mwili wa yesu .basi alfajiri na mapema siku ya jumapili,walifika kaburini,jua lilipoanza kuchomoza”.
MARKO 16:1-2(BIBLIA-HABARI NJEMA, KISWAHILI CHA KISASA)
Hivyo hapo na habari ya ufufuko wa Yesu,tunaona kuwa alifufuka jumapili amboyo ndiyo siku ya kwanza  ya juma  soma MATHAYO 28:1

Ø  Pia biblia inatuonyesha siku ya kifo chake,ilikuwa ijumaa ambayo ndiyo maandalio ya sabato.
“Siku hiyo ilikuwa ijumaa,na maandalio ya siku ya sabato yalikuwa yanaanza .wale wanawake  walioandamana na yesu kutoka  Galilaya walimfuata Yosefu, wakaliona lile kaburi na jinsi mwili wake Yesu ulivyowekwa .Halafu wakarudi nyumbani,wakayatayarisha manukato na marashi ya kuupaka mwili wa Yesu .Siku ya sabato walipumzika kama ilivyoamriwa na sheria”LUKA 23:54-56

(BIBLIA TOLEO LA HABARI NJEMA KISWAHILI CHA KISASA)
Kwahiyo tunaona kuwa sabato siyo ijumaa wala Jumapili bali ni Jumamosi
5. Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa   BWANA Mungu wako.KUTOKA 20:12
6. Usiue. KUTOKA 20:13

7. Usizini. KUTOKA 20:14

8. Usiibe. KUTOKA 20:15

9. Usitoe ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yako. KUTOKA 20:16
10. Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ng’ombe wake au punda wake wala cho chote kile alicho nacho jirani yako. 

KUTOKA 20:3-17, KUMBUKUMBU LA TORATI 5:7-21
Ø  Amri za Mungu ni za muhimu kwa Nyakati zote na vizazi vyote.Yesu anatoa agizo hili juu ya umuhimu wa amri za Mungu:-

“……………………….lakini ukitaka kuingia katika uzima zishike amri MATHAYO 19:17
“Msidhani kwamba nimekuja kuondoa Torati au Manabii, sikuja kuondoa bali kutimiza.Kwa maana,amin, nawaambia, mpaka mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata herufi moja ndogo wala nukta itakayopotea kwa namna yo yote kutoka kwenye Torati mpaka kila kitu kiwe kimetimia. Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.Kwa maana nawaambia, haki yenu isipozidi haki ya waandishi wa sheria na Mafarisayo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni”.MATHAYO 5:17-19

Ø  Watu wengi leo ,hutoa udhuru wa kuzishika Amri kumi za Mungu,kwa madai ya kumwamini na kumpenda Yesu.Husema “Ukimwamini Yesu tu,inatosha,hakuna haja ya kuzishika amri”.je, udhuru huo Yesu aliukubali katika maandiko matakatifu?

Yesu mwenyewe alisema;-
“Mkizishika amri Zangu mtakaa katika pendo Langu, kama Mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo Lake.”YOHANA 15:10
“Kama mnanipenda, mtazishika amri Zangu.”YOHANA 14:15
“Kwa kuwa huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzitii amri Zake. Nazo amri Zake si nzito”.1YOHANA 5:3

Ø  Je amri za Mungu kila mtu anapaswa kuzijua na kuzishika? Au kwa ajili ya watu Fulani tu,au dhehebu Fulani tu?
Biblia Inasema:-
“Hii ndiyo ya maneno ;yote yamekwesha sikiwa,mche mche Mungu, nawe uzishike amri zake maana kwa jumla ndiyo impasavyo mtu “MHUBIRI 12:13

Hivyo tunaona kuwa biblia inasema kuzishika amri za mungu kunampasa kila mtu yeyote anayejifahamu kuwa yeye ni mtu ‘ anapaswa kuzishika amri za mungu. Hata kama mtu angesema’Mima nampenda mungu’ au mimi nimeokoka; kama bado hataki kuzishika Amri za mungu ;madai yake huyo hayaungwi mkono na Biblia kwan maandiko yanasema”

Wokovu u mbali na wasio haki’ kwa maana hawajifunzi amri zako ZABURI 119:115
‘’Umewakataa wote wazikosao amri zako ,kwa maana hila zao ni uongo’’ZABURI 119:118
‘’Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye ikiwa tunashika amri zake.Yeye asemaye nimemjua ,wala hazishiki amri zake,ni uongo wala wala kweli haimo ndani yake’’YOHANA2:34.MITHALI28:9

Ø  Kwa hiyo hapana maandiko yatwambia kuwa,kutozitii amri za mungu nab ado huku tukijiita wakristo,Watu wa mungu Wanaompenda Mungu ,Walio okoka, Washika ibada na majina mengine kama hayo ya kujisifia uumini Huku tunapinga na kuvunja amri za mungu Maandiko yanasema watu wa namna hiyo ni ‘’WAONGO’’NA tunajua kuwa mwongo hawezi kwenda mbingni (soma ufunuo 21;8,22;15)Maana uongo bado ni uvunjaji wa amri ya tisa (KUTOKA 20;16)Katika amri kumi za MUNGU            
                                
Wengi wamefundishwa kuzishika amri baadhi na zingine kuziacha,na kutoa mafundisho kuwa eti hizi hazituhusu,maana ziliondolewa na yesu pale msalabani n.k kwa mfano,amri ya pili inayokataza ibada ya sanamu (KUTOKA 20:4-6)NA amri ya nne inayo waigiza watu waitunze sabato siku ya saba ya juma (KUTOKA 20:8-11)amri hizi zimevunjwa wazi na kuondolewa na watu mamilion wanafundishwa na viongozi wao wa makanisa kuwa amri hizo kwa sasa haziwahusu.Huu ni mpango mkuu wa Yule adui (SHETANI)kuwafanya watu wamwasi Mungu kwa kuzivunja amri zake.                         
BIBLIA YENYEWE ANATOA ANGALIZO HILI:-                                                  
“Maana mtu awe yote atakaye shika sheria yote ila akajikwaa katika neon moja amekosa juu ya yote kwa maana yeye alisema,usizini,pia alisema usiue.Basi ijapokuwa hakuzini lakini umeua umekuwa mvunja sheria. Semeni ninyi na kutenda kama watu watakao hukumiwa kwa sheria ya uhuru’’YAKOBO 2:10-12, SOMA PIA, MATHAYO 5:19      
Kwa  nini watu wengi wachague kuvunja amri za mungu na hali ya kuwa amri ziko wazi katika neon lake –maandiko matakatifu.?       
                
Biblia ainatoa sababu ya uvunjaj I wa sheria hizo za mungu kauli ya yesu iliyo sema:-   
Akawambia ,isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki kama ilivyo andikwa,watu hawa huniheshimu kwa midomo ,ila mioyo iko mbali name:Nao waniabudu bure wakifundisha mafundisho yalio maagizo ya wanadamu.       
Ninyimwaiacha amri ya mungu na kuyasniks mapokeo ya wanadamu .Akawaambia vema mwaikataa amri ya mungu mpate kuyashika mapokeo yenu’’ MARKO 7:6-9

Ø  Biblia inatwambia sababu ya wengi kuvunja amri za mungu ni mapokeo ya wazee(VIONGOZI)wengi leo wanafundishwa mapokeo ya wanadamu na kuyatii kwa uaminifu kuliko amri za mungu ,hata kama mapokeo hayo hawayapatii ushindi wa maandiko hutetea kwa msimamo mkali wa kulinda itikadi za madhehebu kwa hiyo Miongozo,kanuni,katiba,desturi na heshima kwa viongozi wanadamu vimechukua nafasi kuliko maandiko matakatifu yaliyo neon laMungu.   

Ø  Ndugu msomaji mpaka haoa utakuwa umegundua umuhimu wa kuzijua na kuzitii amri kumi za mungu amua kuishi kulingana na matakwa ya mungu katika amri zake. Kwani kuna mbaraka mkubwa katika kuzishika amri maana Neno la MUNGU lasema,   
“Aishikaye amri hatajua neon baya na moyo wa mwenye hekima hujua wakati na hukumu MHUBIRI 8:5         

Ø  Tena watu wa mungu waaminifu watatambuliwa tu kwa kuzishika amri za mungu na si vinginevyo hivi ndivyo neon la Mungu linavyothibitisha kwa kusema    
   ’’Na waende kwa sheria na ushuda ikiwa hawasemi sawasawa na neon hili bila shaka kwa hao hapana asubuhi  ASAYA 8:20     
        
 ’’Hapa ndipo penye subira ya watakatifu hao wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu’’UFUNUO 14:12                      
                                      HITIMISHO  
Katika kuzishika amri za  Mungu ,mwanadamu anaweza kuishi kwanzo.Ndivyo nenola mungu linavyosema ,    
“Naye akanifundisha ,akaniambia ,moyo wako uyahifadhi maneno yangu shika amri zangu ukaishi”  MITHALI 4:4        

“ Nikawapa amri zangu na kuwaonyesha hukumu zangu ambazo mwanadamu ataishi kwazo. Kama akizitenda” EZEKIEL 20:11      
“Naye akaandika juu ya mbao mfano ya maandiko ya kwanza zile amri kumi alizo waambia bwana huko mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano ; Bwana akanipa”KUMBUKUMBU LA  TORATI  10:4   

“Bali agano hili ndilo natakalo fanya na nyumba ya Israeli,baada ya siku zile,asema Bwana;nitatia sheria yangu ndani yao na katika mioyo yao nitaiandika;name nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.”YEREMIA 31:33
“Mwanangu, shika maneno yangu na kuyahifadhi maagizo yangu ndani yako.Shika maagizo yangu nawe utaishi, linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako. Yafunge katika vidole vyako,yaandike katika kibao cha moyo wako.”MITHALI 7:1-3

No comments:

Post a Comment