.

.

.

.

Friday

Ufahamu juu ya ugonjwa sugu wa Figo


Siku ya figo Duniani inalenga kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa figo zetu, afya zetu kwa ujumla na kupunguza uwepo na matokeo ya magonjwa ya figo na vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo. Katika maadhimisho ya siku hii Dkt. Kavita Parihar, mkuu wa “Nephrology” na idara ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Apollo, Ahmedabad anawatahadharisha Watanzania juu ya dalili, hatari, matatizo, matibabu na uzuiaji kuhusiana na ugonjwa huu.

Ugonjwa sugu wa figo (CKD – Chronic Kidney Diseases), ambao unajulikana pia kama kushindwa kwa figo, ni ugonjwa unayo athiri figo hatua kwa hatua na kusababisha kushindwa kufanya kazi. Wakati ugonjwa sugu wa figo unapofikia hatua ya juu, majimaji hatarishi, elektroliti na taka zinajijenga katika mwili.

Katika Afrika, Magonjwa sugu ya figo huathiri watu wazima hasa vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 50, na hasa ni kutokana na magonjwa ya presha na “glomerular”, tofauti na nchi zilizoendelea, ambapo CKD inasumbua zaidi wagonjwa wenye umri wa kati na wazee na utokana na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu. Dalili uchelewa kujionesha, 75% katika watu wanayo fikia hatua za mwisho za magonjwa ya figo (ESRD) wanahitaji uchunguzi zaidi. CKD inatokea mara 3-4 zaidi katika Afrika kuliko katika nchi zilizoendelea

Magonjwa na hali ambayo mara nyingi inasababisha ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na:

Kisukari
Shinikizo la damu
Magonjwa yanayoshambulia kinga ya mwili (kama lupus, VVU na IgA neforopathy)
Ugonjwa wa figo lenye uvimbe
Kuziba muda mrefu kwa njia ya mkojo, kutokana na hali kama vile kibofu kuwa kikubwa, mawe ya figo na baadhi ya saratani

Mambo yanayoweza kuongeza hatari ya ugonjwa sugu wa figo ni pamoja na:

Ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu, cholestrol kuwa juu na ugonjwa wa moyo
Uvutaji sigara na uzito kuzidi
Kuwa na asili ya Afrika, Marekani au Asia
Historia ya ugonjwa wa figo kwa familia
Umri wa miaka 65 au zaidi
Dalili za ugonjwa wa figo:
Kichefuchefu, kutapika na kupoteza hamu ya kula
Uchovu na udhaifu
Matatizo ya usingizi, kupungua uwezo wa akili na misuli kufyatuka / kukaza
Mabadiliko katika mkojo na uvimbe wa miguu na vifundoni
Kukosa pumzi, maji kujaa katika mapafu
Shinikizo la damu (presha) bila kua na uwezo wa kudhibiti

Ugonjwa sugu wa figo unaweza kuathiri karibu kila sehemu ya mwili. Athari ni pamoja na:

Kuhifadhi majimaji (Fluid retention)
Kupanda ghafla kwa potasium katika damu
Mifupa dhaifu, hatari ya mipasuko kwenye mfupa na upungufu wa damu
Kupunguza hamu ya tendo la ndoa au kupoteza uwezo kabisa
Uharibifu wa mfumo wa fahamu
Kupungua utendaji wa kinga ya mwili, ambayo inafanya kuwa katika hatari zaidi ya maambukizi

Matibabu
Matibabu yana hatua mbali mbali za kusaidia kudhibiti dalili, kupunguza athari, na kupunguza kasi ya maendeleo ya ugonjwa huo. Kama figo likiwa limeharibiwa vibaya, mtu atahitaji matibabu ya hatua za mwisho ya ugonjwa wa figo.

Namna ya kujikinga
Pata tiba yashinikizo la damu
Tiba ya kupunguza kiwango cha cholestrol.
Dawa za kutibu upungufu wa damu. Dawa ili kupunguza uvimbe
Tiba ya kulinda mifupa.
Kupunguza ulaji vyakula vyenye protini ili kupunguza taka katika damu.

Matibabu kwa hatua za mwisho wa ugonjwa wa figo

Katika hatua za mwisho wa ugonjwa wa figo, matibabu ya kitaalamu yajulikanayo kama “dialysis” au kupandikiza figo hunahitajika. “Dialysis” hasa huondoa bidhaa taka na maji ya ziada katika damu wakati figo haiwezi tena kufanya hivi. Katika “hemodialysis”, mashine huchuja taka na majimaji ya ziada katika damu. Katika “peritoneal dialysis”, mrija mwembamba (catheter) uingizwa katika tumbo kisha kujazwa na majimaji yanayo nyonya uchafu. Baada ya muda majimai haya yatoka mwilini yakibeba uchafu huo.
Upandikizwaji wa figo
Upandikizaji unajulikana kama "Zawadi ya Maisha" kwa sababu inaokoa maisha na kurejesha ubora wa maisha kwa wale ambao wamekuwa wagonjwa kwa muda mrefu. Upandikizaji una faida nyingi, hupunguza haja ya “dialysis” na husaidia wagonjwa kufurahia maisha na kuwa huru zaidi. Ingawa wagonjwa wengi hufanyiwa dialysis kabla ya uchunguzi zaidi kwa upandikizaji, wagonjwa katika hatua za mwisho za ugonjwa wa figo wanaweza kufanyiwa upandikizaji hata kabla ya kuanza “dialysis”.
Mafanikio katika upandikizaji wa figo hutibu na kurudisha afya katika viungo hivo. Pamoja na hiyo huleta afya na maisha bora ndio maana ni matibabu yanayopendelewa na wagonjwa wengi. Kawaida kutakuwa na vizuizi vichache juu ya unywaji wa vinywaji na chakula baada ya kufanyiwa upandikizaji. Wagonjwa wengi pia hurudi kufanya kazi na kuishi maisha kamili baada ya operesheni hiyo..
Jinsi ya kuzuia Kushindwa kwa figo

Udhibiti wa ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu
Kupunguza ulaji wa mafuta na chumvi
·         Kufanya mazoezi kila siku za wiki
Kufanya uchunguzi wa mara kwa mara
Kuzuia utumiaji wa tumbaku
Kuzuia utumiaji wa vilevi
Kuepuka utumiaji wa dawa pasipo maelekezo ya daktari

Dr Kavita Parihar ni mtaalamu katika magonjwa ya figo amepata mafunzo ya magonjwa ya figo  na upandikizaji figo kutoka taasisi maarufu India, ana uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini. Alianzisha idara ya magonjwa ya figo na programu ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Apollo, Ahmedabad, India mwaka 2003. Hivi sasa yeye ni kiongozi wa idara ya magonjwa ya figo  na kupandikiza figo katika Hospitali ya Apollo, Ahmedabad. 


Dkt. Kavita Parihar

MBBS, MD (Medicine) DNB (Nephrology)

No comments:

Post a Comment