.

.

.

.

Thursday

Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo wamekoleza moto kuikataa Katiba

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri la Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa 
Gazeti la Mwananchi la Machi 13, 2015 lilibeba ujumbe mzito kwa Watanzania. Kichwa cha habari kimoja kilisomeka: “Maaskofu: Pigieni Katiba kura ya hapana.”

Maaskofu wa Jukwaa la Wakristo ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT) Askofu Daniel Awet, kwa sauti moja wamewataka waumini wao kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Wapigakura, kuisoma vyema Katiba Inayopendekezwa na hatimaye kuikataa kwa kuipigia kura ya ‘hapana.’

Sababu kuu za kuwahamasisha waumini wao na Watanzania kuikataa Katiba Pendekezwa ni mbili. Mosi ni kulazimisha kura ya maoni ya katiba mpya kufanyika bila maandalizi ya kutosha, yakiwamo maridhiano ambayo yameligawa Taifa katika vipande vipande.

Pili viongozi waandamizi wa Serikali ya CCM kuupigia debe muswada wa Mahakama ya Kadhi.

Tamko hili nyeti ambalo limesambaa katika makanisa mengi iwapo litasomwa kwa waumini wote na kuhamasishwa na mapadri, wachungaji na wainjilisti basi unaweza ukawa ndiyo mwisho wa Katiba Inayopendekezwa kupigiwa kura Aprili 30 mwaka huu.

Viongozi wa jukwaa hilo wana wajibu wa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuandika Katiba Mpya ambalo linawahusu waumini wao pia. Katiba siyo suala la siasa, bali ni la Watanzania wote.

Itakumbukwa kuwa CCM ilitumia mabavu na fedha nyingi katika kusimamia mijadala ya Katiba Mpya, wakapitisha Katiba kwa kutumia vyombo vya dola.

Hofu ya kukataliwa kwa Katiba Mpya kumeifanya Serikali ya CCM ivunje kabisa makubaliano na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwamba Kura ya Maoni ingesitishwa hadi baada ya uchaguzi 2016.

Hata hivyo, kwa sababu ya hofu ya kuanguka madarakani, CCM imeamua iendelee kulazimisha kura ya maoni kwa kutumia mabavu na hivyo kuwaburuza wananchi.

Matokeo yake Serikali ya CCM inafanya kila hila ili Daftari la Wapigakura lisiboreshwe ili waweze kuchota kura vizuri kiholela holela.

Nionavyo hofu kuu ni Katiba hii kuja kukataliwa na umma, hivi Rais Kikwete ameona heri aendelee kuisukuma walao ikubalike na umma. Lakini ukweli ni kwamba katiba hii imekataliwa na wananchi wengi pia hata na Mungu kwa sababu ‘sauti ya wengi ni sauti ya Mungu’.

Sababu nyingine kubwa ya kukataliwa na wananchi wakiwamo maaskofu ni Katiba Inayopendekezwa kulenga kulinda masilahi ya watu wachache ndani ya chama na Serikali ya CCM.

source:mwananchi

No comments:

Post a Comment