Hofu:- Ni kuogopa mambo yaliyopita, yaliyopo au yajayo. Kibiblia : hofu ni kukosa imani! “ mwenye haki wangu ataishi kwa IMANI naye akisitasita roho yangu haina furaha naye” (waebrania 10:38) neno “kusitasita AMPLIFIED BIBLE inasema “draws back or shrinks in fear” unaona sasa Hivyo imani ni kinyume cha hofu! Kibiblia.
Aina tatu za Hofu;
1) Kuogopa mambo yaliyopita!
Watu wengi wapo kwenye hofu leo kutokana na mambo waliyopitia zamani,
Mfano : Dhambi walizotenda zamani , uongo waliofanya zamani n.k. nao wanaishi
katika hofu kwa kuwaza, je kweli Mungu atawasamehe , watu watawachukuliaje?,
watarudi kwenye hali ya mwanzoni? Lakini biblia inasema “hata imekuwa mtu akiwa
ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa mapya”
(2Kor 5:17).
2) Kuogopa mambo yaliyopo!
Kutokana na hali ngumu ya maisha watu wengi wamejikuta kuishi kwenye hofu ya
mambo yaliyopo hii inatokana na watu wengi , kuangalia hali wanayopitia bila
kushirikisha uweza wa Mungu na hii inasababishwa na mtu kukosa muda wa kumtafakari
Mungu na neno lake. biblia inasema “kitabu hiki cha torati kisitoke kinywani
mwako bali yatafakari maneno yake mchana na usiku ,ukapate kuangalia kutenda
sawasawa na maneno yote, yaliyo andikwa humo maana ndipo utakapo ifanikisha
njia yako , kisha ndipo utakapo stawi sana” (Yoshua 1:8)
3)
Kuogopa mambo yajayo!
Kutokana na kutojua ya kesho watu wengi wameingia kwenye hofu ya mambo yajayo,
ila Yesu alitunya mwanzo kuwa “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake
na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho itajisumbukia yenyewe.
Yatosha kwa siku maovu yake” (Mathayo 6:33-34)
Vyanzo vya Hofu (kibiblia)
Kutokuwa na mwongozo wa Roho mtakatifu!
Kukosa mwongozo wa Roho mtakatifu kutakufanya ukose uhakika wa pale unapoelekea
na ndio maana Yesu alisema “lakini mtakapo pelekwa pelekwa, msifikiri fikiri
mtakayo sema , maana mtapewa saa ileile mtakayosema ,. Kwa maana si ninyi
msemao bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu” Mathayo 10:19-20 , kukosa
mwongozo wa Roho kuna mletea mtu hofu na kushindwa kuamua.
Kutokufunga na kuomba
Mtu asiyeishi maisha ya maombi anakuwa na imani dhaifu, ambayo inasababisha
hofu, tunajifunza Yesu alipoona mateso anayoyaelekea kuwa ni mazito sana,
akachukua hatua ya kuomba Yesu alijua hofu ni dhambi na kuyaogopa mateso ni
dhambi akaamua kushindana dhambi hiyo hadi kutoa machozi ya damu, biblia
inasema “hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi” Waebrania
12:4, Yesu alipambana kuishinda dhambi ya hofu! Lazima tupambane na hofu!
Kutokusoma na kutafakari neno la Mungu
Mtu asiyesoma neno la Mungu imani yake inakuwa ndogo, ambayo haijalishwa neno
la kutosha, mfano wa Petro, alimwona Yesu anaelea kwenye maji akataka kumfuata
Yesu akamwambia njoo, katikati akaona shaka akataka kuzama sasa angalia maneno
ya Yesu “Mara Yesu akamshika mkono akamwambia , Ewe mwenye imani haba , mbona
uliona shaka” uhaba wa imani unasababishwa na upungufu wa maneno ya Mungu,
ukisoma neno la Mungu unaikuza imani yako na kwa kutafakari unaimarisha
ulichoingiza! Hapo hofu itakosa nafasi kwako kabisa!
Kitokuwa na Imani
Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo , ni bayana ya mambo yasioonekana
kwa macho. Kutokuwa na imani ni kutokuwa na uhakika wa mambo ya tarajiwayo, hii
ni sababu moja wapo ya hofu kama tulivyoona hapo juu. Watu wengi wameishi
kwenye mateso kwasababu ya hofu yamkini hata wanaomwamini Yesu kristo! Hii ni
kukosa imani na kuishi maisha yasiyoya imani ni dhambi mbele za Mungu! “kwa
kuwa tendo lolote lisilotoka katika imani ni dhambi” 1kor 14:23
MADHARA YANAYOSABABISHWA NA HOFU
Unakuwa mtumwa
Hofu inaweza kumfanya mtu akawa mtumwa , biblia inasema “….mlipokuwa watumwa wa
dhambi…..”warumi 6:17,20 , hofu ni dhambi ambayo inatuweka katika utumwa ,
utahofia kila kitu , kila mtu n.k. umelala unasikia kitu kinapiga kelele nje unajikuta
umeogopa, utumwa! Ila Yesu alituokoa kutoka kwenye utumwa wa hofu “maana Kristo
naye alikufa ili kwa njia ya mauti amwaribu yeye aliyekuwa na nguvu,ili awaweke
huru wale ambao maisha yao yote kwa sababu ya hofu ya mauti walikuwa katika
hali ya utumwa” Ni kumdharau Mungu na neno lake
Hofu ni kumdharau Mungu na neno lake, kwenye biblia neno usiogope limeandikwa
zaidi ya mara 365, hii ni kuonyesha hofu haitakiwi “…maaana hofu ina adhabu…”
kwahiyo hatutakiwi kuwa na hofu, kabisa! “….maana mwenye shaka ni kama wimbi la
bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku” Yakobo 1:6 Maombi yako hayatajibiwa
“Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kutoka kwa Bwana” Yakabo
1:7 hivyo hofu huzuia maombi yako yasijibiwe, na Mungu kwahiyo yanakuwa kama
kelele tu! Wala Mungu hayajibu jiulize ushaomba mara ngapi ukiwa na hofu
ukajibiwa?
Itakupelekea kutupwa Jehanum
“Bali waoga , na wasioamini na wachukizao,na wazinzi, na wachawi…..sehemu yao
ni katika lile ziwa liwakalo moto na kibiriti..” ufunuo 21:8 . unaona wenye
hofu ndo miongoni wa watu wa mwanzo kutupwa Jehanamu, Hofu ni dhambi yenye
uwezo wa kukupeleka motoni jiangalie maisha yako yakoje je unaishi katika hofu?
biblia inasema “Basi msiutupe ujasiri wenu, maana una thawabu KUU” neno KUU lina
maana sana hapo!
Nitatokaje kwenye maisha ya Hofu.
Hofu haikutoka kwa MUNGU “MAANA Mungu hakutupa Roho ya hofu , bali ya nguvu na
ya moyo wa kiasi” 2 timotheo 1:7 Kama tulivyoona hofu ni dhambi, kama ni dhambi
unatakiwa uchukue hatua ya kutubu kwanza kutoka ndani, halafu uichukie kabisa
hofu, kutubu huku kunatakiwa kuendane na kuanza kusoma neno la Mungu na
kulitafakari, kufunga na kuomba ili kupata nguvu ya kuishinda hofu! Mwombe Roho
mtakatifu akupe ujasiri zaidi na zaidi, utaona maisha yako yatabadilika utaanza
kumuona Mungu yuko karibu na maisha yako! KUMBUKA BAADA YA KUTUBU USIRUDI TENA
KWENYE UTUMWA WA HOFU!!! UBARIKIWE,
e-mail:
No comments:
Post a Comment