Lillian Lewis |
Pamoja na maamuzi hayo hofu imetanda kuwa huenda mtandao huo umegawanyika ukatengwa na Vatican.
Kwenye miaka ya 1960, Liliam alikuwa katika orodha ya wanawake wa kwanza wa Katoliki kushiriki masomo ya theolojia. Mara baada ya kusimikwa kwake, mwanamke huyo alinukuliwa na BBC akisema, “Kashfa zilizoliandama kanisa Katoliki duniani katika miaka ya hivi karibuni, ni miongoni mwa mambo yaliyonifanya niingie katika utumishi
“Nimedhamiria kuonesha kwamba wanawake tuna nafasi kubwa ya kuongoza kama makasisi. Nina mabinti wanne. Hakuna hata mmoja ambaye anasali kanisa Katoliki kutokana na mwenendo wake”
Hafla maalumu ya kumpa Upadre mwanamke huyo, iliyofanyikaa Jumamosi iliyopita ilihudhuriwa na wageni 200 waliokusanyika nyumbani kwake, wakitokea madhehebu mbalimbali ya kidini, kasoro viongozi wao wa Kikatoliki.
Padre huyo ambaye ni mwanachama wa mtandao wa Roman Catholic Women priests ulioanzishwa mwaka 2001, umoja wao umekuwa ukitaka ushirikishi wao ndani ya Kanisa Katoliki, ili kumjua na kumtumainia Kristo zaidi kwenye karne hii ya 21.
Viongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Michigan, ambao hawakuhudhuria sherehe hizo, walieleza kuwa waumini wao walioshiriki kwenye sherehe hizo batili, nao watashughulikiwa.
Askofu Paul Bradley wa Jimbo Katoliki Kalamazoo, alitoa tamko kali kupitia mtao wa WWWMT-TV in Kalamazoo, Mich, akieleza kuwa yeyote aliyeshiriki shughuli hiyo, kamwe hatambuliwi na Kanisaa Katoliki.
Mbali na kuonywa na Jimbo hilo, Lewis alisema shughuli hiyo ilikuwa yenye mafanikio na alitarajia kuwa ingepingwa na Kanisa Katoliki. Hata hivyo, alisema licha ya kupewa daraja hilo, hafahamu jukumu ambalo atapewa na kanisa.
Alisema majirani zake na wanawake wa kiume na mchumba wake, walimuunga mkono baada ya kutambua nafasi ya mwanamke kama kasisi na kusema yuko tayari kuwafungisha ndoa wapenzi hao.
Mashirika mbalimbali ya kitaifa, yamedai kuwa hiyo ni changamoto kubwa ndani ya kanisa hilo kwa sasa, kwani na Mapadre wanaume nao wamekuwa na kilio cha kutaka wapewe fursa ya kuoa, licha ya Papa Francis kuonekana kuwa na upinzani katika hilo.
No comments:
Post a Comment