Maandalizi ya Mkesha wa AFLEWO (Africa Lets Worship) 2014 Maandalizi yakamilika.Mandalizi hayo yaliyoanza tangu mwaka jana kwa usaili wa wanakwaya na ikifuatiwa na mazoezi ya Kuimba na Wanamziki kutoka Makanisa mbalimbali Jijini Dar es salaam.
Mpaka sasa maandalizi tayari yamekamilika kinachosubuliwa na muda kesho saa 3:00 usiku katika Kanisa la City Christian Center Upanga(CCC)
karibu na Chuo cha Mzumbe,Siku ya Ijumaa 13/06/2014.
Mkesha huo wa Kusifu,Kuabudu na Maombi kwa
ajili ya Afrika na Tanzania utakuwa na Waimbaji zaidi ya hamsini kutoka Makanisa
mbalimbali watakuwa kwenye jukwaa moja wakimsifu
Mungu
Waumini,Wachungaji na Maaskofu watakusanyika kumwomba Mungu hasa
kwa mchakato mzima wa Katiba mpya na Uchaguzi mkuu 2015.Hakuna Kiingilio.
Mawasiliano:
+255712207717
Dr Ona Machang'u Kiongozi wa Sifa katika Mazoezi ya AFLEWO 2014 |
AFLEWO Mass Choir 2014 Katika Mazoezi |
No comments:
Post a Comment