Mainjinia wa kivita wa Israeli wamekamilisha mipango yote ya kulivamia taifa hilo la kiislamu ili kulipokonya uwezo wa kumiliki silaha za nyuklia, huku mpango vita ukionesha kuwa idadi ya wayahudi watakaopoteza maisha vitani na wale watakaofikiwa na makombora ya masafa marefu yakiwepo Scud watafikia 500, huku mapigano yakikadiriwa kuchukua siku 30.
Waziri wa Ulinzi wa Israel, alibainisha hayo wiki iliyopita alipokuwa akiongea na Gazeti la Maariv la nchini humo, ambapo alieleza kwamba wanatarajia kufanya uvamizi dhidi ya taifa la Iran mapema mwezi huu wa Oktoba, na wataanzisha vita vitakavyodumu kwa siku 30, na hilo litapelekea waisrael wasiopungua 500 kupoteza maisha.
Inaelezwa kuwa waraka huo unaweza kuwa umeachiwa uvuje kama onyo la mwisho kwa mataifa ya magharibi yanayosua sua kuidhibiti Iran na kuipokonya uwezo wa kumiliki silaha hizo za maangamizi makubwa.
Mmoja wa wataalamu hao walioteuliwa kuandaa mpango vita (jina linahifadhiwa) alisema kuwa mapigano Jeshi la Israeli lina utayari wa vita kuliko wakati mwingine wowote wa uhai wake na halina cha kusita linasubiri amri ya utekelezaji kutoka kwa Waziri Mkuu tu.
Kulingana na mpango huo, shambulia la kwanza litahusisha makombora ya kurushwa kutoka baharini kwenye manuari zinazotumia vipimo vya setilaiti, yakipiga maeneo 100 kwa wakati mmoja yakiwepo yale ya vituo vya kurushia makombora kambi za jeshi na miundombinu muhimu ya kivita na mashambulizi hayo yatakuwa mfululizo nchi nzima kwa saa 48, kisha ndege vita zisizo na marubani 500, zitaruka kwa pamoja kwenye anga ya irani na kuleta maangamizi makubwa.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin wa Netanyahu |
Hata hivyo maafisa wa Irani kwa utafiti wao walioufanya walibaini kuwa, Jeshi la Israeli limejipanga vilivyo kupambana na Iran na wamejipanga ili kukabiliana nao ikiwezekana kuwazuia ingawa wanakiri kuwa taifa hilo linateknolojia ya hali ya juu sana hasa katika uwezo wake wa angani.
Nyaraka za siri za Israeli zimeeleza kuwa, oparesheni ya kijeshi itaanza kuharibu miundo mbinu ya Iran ikifuatiwa na kuteketeza silaha za kivita kwa kutumia silaha na kumalizikia kwenye vinu vya kinyuklia zilizotengenezwa na wao.
Marekani na marafiki zake wamekuwa katika juhudi kubwa za kuhakikisha kuwa zinazuia shambulio la kivita kutoka Israeli kwa kumaliza mgogoro huo kwa amani, ingawa kikwazo ni mataifa ya Urusi na China ambayo yamegoma kupitisha azimio kali linaloweza kuilainisha Iran.
Rais wa Irani Ahmadinejad |
Mwanadiplomasia makini, Jonathan Marcus akielezea uvamizi huo unaotarajiwa kufanywa na Israel alisema; mbali na ndege zisizokuwa na rubani, lakini pia kutakuwa na zana zingine ambazo hakutaka kuziweka wazi kwa kuwa mwisho wa zoezi litaleta hasara kubwa nchini Iran.
Serikali ya Iran na jeshi lake ilisema wazi kuwa, kama litashambuliwa na Israel au Marekani, italipiza kisasi kwa njia isiyotarajiwa katika malengo ya mataifa ya maghari kote dunia na kwa hakika dunia itakuwa mahali pachungu pa kuishi kwa kila mtu.
Akiongea katika mahojiano na Gazeti la Maariv, Jenerali mmoja aliyestafu mwezi wa nane, mwaka huu na kupelekwa kuwa balozi wa nchi hiyo huko China, aliyejitambulisha kwa jina moja la Vilnai alisema, Israel imejiandaa kwa viwango vya juu tofauti na maandalizi yaliyopita.
Jumanne iliyopita, Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu alisema, matatizo ya kinyuklia yalipelekea Irani kushindwa kufikia makubaliano na nchi nyingine zenye nguvu duniani zilizokuwa zikipinga mpango huo wa kinyuklia.
Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak |
Waziri wa ulinzi, Ehud Barak na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu walipinga vikali maoni ya viongozi wa Wizara ya Ulinzi kwamba waanzishe mashambulizi dhidi ya Iran kwa siri.
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, na Ehud Barak walieleza kwamba katika vita itakayotokea kati ya Israeli na Iran, hoja kubwa ni kutafuta uhalali ili kuwavuta Marekani katika vita.
“Mpango ni mwepesi, Netanyahu na Barak wa Israel wana nguvu za kijeshi kuishinda Iran kutokana na zana zake za kinyuklia. Na lazima wapigane ili kukwamisha mpango wa Iran wa kutengeneza silaha za kinyuklia,” alisema mmoja wa wachambuzi makini.
Rais wa Marekani atakuwa hana uchaguzi ila kuliagiza jeshi lake kujiunga kupigana vita. Netanyahu alisema kwamba, kama Obama hataki kufanya hivyo, atashindwa katika uchaguzi na Romney atashika nafasi yake.
No comments:
Post a Comment