Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi ambaye pia ni Katibu mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Florence Turuka ametangaza wajumbe 201 watakao wakilisha wajumbe kwenye Bunge la Katiba linalotarajiwa kufanyika Februari 18 mwaka huu.
Wajumbe hao wamegawanyika katika makundi 10 ambao kati ya hao,kundi
la wajumbe 20 litawakilisha taasisi za Dini katika Bunge hilo.
Taasisi nyingine ni pamoja na Taasisi zisizokuwa za Kiserikali wajumbe (20)Vyama vyote vya kisiasa vyenye usajili wa kudumu(42),Taasisi za elimu (20),Watu wenye ulemavu (20), Vyama vya wafanyakazi (19),Vyama vinavyo wakilisha wafugaji(10), Vyama vinavyo wakilisha wavuvi(10), Vyama vya wakulima(20) naVyama vya watu wenye malengo yanayofanana(20)
Makundi hayo yanajumuishwa na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na ufanya idadi ya wabunge wa Bunge la Katiba kufikia 64.Kwa upande wa taasisi za Dini kwa upande wa Tanzania Bara (13) ni Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dr.Donald Leo Mtetemela,Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Ernest Kadiva amabaye pia ni Katibu mkuu Utawala,Utumishi na Milki waDayosisi ya Mashariki na Pwani.Wengine ni Profesa Costa Rick Mahalu,Mussa Yususfu Kandecha,Askofu Amos J .Muhagachi,Magdalena Songora,Sheikh Hamid Masoud Jongo,Shamim Khan,Tamrina Manzi,Respa Adam Miguma,Easter Msambazi,Hamis Ally Togwa,Olive Damian Luwena.
Kwa Upande wa Tanzania Zanzibar (7) Shekh Thabit Nouman Jongo,Shekh Nassoro,Shekh Nassoro Mohamed Ibrahimu,Louis Majaliwa,Suzana Peter Kunambi,Fatma Mohammed Hassan na Yasmin Yusufali E. Halloo.
Awali taasisi za kidini zilizo peleka mapendekezo li kuchaguliwa kuingia kwenye Bunge la Katiba kwa Upande wa Tanzania Bara zilikuwa 246 na upande wa Zanzibar zilikuwa 98.Idadi ya watu waliopendekezwa kuingia katika Bunge la Katiba Tanzania Bar walikuwa 1,203 ambao ni watu 13 tu ndio waliopata nafasi ya kuchaguliwa.Kwa upande wa Zanzibar watu waliokuwa wamependekezwa na taasisi zao waliuwa 444, ambao wajumbe (7) kati ya hao ndi walioweza kupata nafasi ya kweda kutoa mchago katika Bunge hilo
No comments:
Post a Comment