.

.

.

.

Monday

"Kama Serikali tunatambua blogs kama vyombo rasmi vya habari" Dk. Abbas Hassan Mkurugenzi Mkuu Habari Maelezo

Serikali kupitia taasisi yake ya habari maelezo imesema inatambua blogs kama rasmi vya habari , taarifa hiyo imesemwa leo na  Dk. Abbas Hassan Mkurugenzi Mkuu Habari Maelezo alipopata kuzungumza na wamiliki na wanachama wa Blogs nchini wenye chama chao kinachofahamika kama Tanzania Bloggers Network (TBN) 

Dk. Abbas Hassan akizungumza amesema Bloggers wataanza kupata press card na mialiko mbalimbali ya kuhudhulia shughuli za kiserikali na kwa kutambuliwa zaidi Dar es salaam na Mikoani,akamalizia kwa kusema anawaomba maafisa habari wote wa serikali mikoani kutoa 
ushirikiano kwa Bloggers watakaokuja kutaka kupata taharifa za serikali zinazoruhusiwa kutoka.

Mkutano huo umeudhuliwa na Bloggers kutoka ndani ya Jiji la Dar es salaam na Mikoani ikiwa ni kuwakutanisha na kuzungumza na maswali mbalimbali yanayohusu chama chao na mstakabari mzima wa habari kwa njia ya mtandao hasahasa blogs

Bloggers hao walipata muda wa kuzungumza,kuuliza maswali,na kushauriana mambo mbali mbali yanayohusu blogs . 

Story na Tunu Bashemela JR 
 
Dk. Abbas Hassan Mkurugenzi Mkuu Habari Maelezo 
akizungumza Wakati Wa Kufungua Mkutano Mkuu Wa Tanzania Bloggers Network(TBN) Uliofanyika Katika Ukumbi Wa PSPF Jijini Dar.
Dk. Abbas Hassan Mkurugenzi Mkuu Habari Maelezo akizungumza na wamiliki wa vyombo vya habari

Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi(aliyesimama)  akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tanzania Bloggers Network(TBN) 


Source:wazalendo25.blogspot.com

No comments:

Post a Comment