.

.

.

.

Friday

MWL: C. MWAKASEGE SIKU: 5 SOMO: MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO


ENEO: DAR ES SALAAM
▶Lengo
Kuweka maarifa ya Kiblia ndani yako yatakayokuwezesha kutumia FIKRA zako ili ufanikiwe ktk maisha yako

Mith 23:7(a)

HATUA AMBAZO UNAHITAJI KUZIFUATA KAMA UNATAKA KUTUMIA FIKRA ZIKUSOGEZE KIMAISHA

➡Tumeshaangalia hatua 2 tuko tumeanza seminar. Leo tuendelee na ya 3

3⃣Panga FIKRA zako kwa upya ili zisikupitishe tena mahali pabaya ulipokwisha pitia.

✅FIKRA zinapangika
✅Mfano kwa mama mjane baada ya kusaidiwa na Elisha akitaka hali ile ya mwanzo isijirudie tena lazima abadiri kufikiri kwake la sivyo ile hali atarudi tu

2Falm 5:7
Mama mjane alipanga FIKRA zake kwa upya..lazima ujifunze kupanga FIKRA zako kwa upya
Tuonaona mstari wa 7

➡...Nenda kauze mafuta...
Si FIKRA tu kutumika bali MUNGU alitaka Mama mjane ajuaje na akubali ndani yake kuwa MUNGU ndiye amfundishaye kupata faida.

Isy 48:17
✅MUNGU hakufunsidhi tu kuhubiri au kuimba bali pia ukufundisha na upanga FIKRA zako ili zipate kujua MUNGU ndiye akupaye faida

✅FIKRA lazima zipate msaada wa kufundishwa jinsi ya kupata faida

✅Pata tofauti sana kati ya kufundishwa kupata faida na kufundishwa Biashara. Ni sawa na ilivyo tofauti kati ya kufundishwa kufaulu mtihani darasani na kufundishwa juu ya kufaulu mtihani wa kimaisha

✅Maana si kila mtu aliyeko darasani atafaulu maisha, na si kila afanyaye Biashara atapata faida..lazima ujifunze kuvuka hapa

MAENEO MUHIMU YA KUTAKIWA KUBADILIKA

1). Weka FIKRA zako zikubali MUNGU ndiye anayekufundisha kupata faida

▶Watu wengi wakikwama kiroho ukimbilia kanisani ila uchumi wao ukikwama huwaoni kanisani ukimbilia Benki, sasa sisemi Benki ni mbaya au usiende Benki ila wanasahau kuwa

▶ROHO MTAKATIFU ni mwalimu mzuri sana wa kukugundisha ujasiriamali wenye kupata faida

2). Lipa Deni
✅Elisha alimwambia Mama mjane ....kauze kisha lipa deni....

✅Alikuwa anatafuta kitu gani?
▶Alikuwa anapandikiza nidhamu za kutumia fedha ambazo MUNGU amekupa kwa sababu zake alizokupa au ulizomwomba tena kwa mwongozo wake!

▶Mama mjane alikwenda kutaka msaada wa watoto wake kitokuchukuliwa watumwa(Alitaka kupata fedha za kuwakomboa watoto wake)

▶Hakuwa na FIKRA zilizojengeka kulipa deni maana Biblia haituonyeshi aliwahi kukopa. Kama huna FIKRA za kukopa huwezi ukawa na FIKRA za kulipa deni.

Mama mjane alikabidhiwa matumizi ya fedha ktk maeneo haya
⚫Kulipa deni
⚫Gharama za kwake na zile za baadaye
⚫Gharama za watoto na za wakati ule wa baadaye
⚫Kuhakikisha ya kwamba amalizi faida lazima abaki na mtaji.

✳Je unamwomba MUNGU pesa kwa ajili ya nini au kwa ajili gani?
▶Kumbuka pesa uyumbisha mawazo na kujikuta watumia nje ya lile kusudio

▶Ukikorofisha hapo MUNGU ukaa pembeni. FIKRA zinahitaji nidhamu kwenye matumizi ya pesa. Kama MUNGU anakupa kwa ajili ya kitu fulani hakikisha unaielekezea hyo pesa kwenye hicho kitu.

▶Tofauti na hapo utaona ROHO MTAKATIFU anakuhimiza TOBA

Mith 13:22
▶Watu wengi wana FIKRA za kujitazama wenyewe tu kwenye upande wa pesa wanajikuta kusahau kuwa wana familia na watoto!

▶Biblia inatuhimiza kuweka akiba mpaka za wajukuu!

▶Usitazame kukwama kwa mme/mke wako ama wazazi wako, usifike mahali hata pa kuwakasirikia badili FIKRA zako ili wewe uvuke hapo kisha mrushie kamba naye atoke hapo oooh hallelujah Hallelujah

HOME WORK
➡Orodhesha madeni yako

Zab 37:21
✳Umuhimu wa kuorodhesha madeni

▶Usipolipa mikopo MUNGU haji kukupigania katika haki zako.
▶Unapoteza haki katika haki
▶Mikopo isiyolipwa ugeuka deni
▶Deni ubeba vitu (rehani) ili akili zako ziamke. Na baada ya kutaka kuja kuvichukua ndipo akili zako zitaamka
▶Si kila ambaye anashindwa kulipa deni hana hela bali hana mpangilio mzuri wa matumizi na ulipaji

Yer 22:21
✅Si kwamba hapendi kusikia bali hataki kusikia maana yake hataki kutekeleza alichoambiwa

✅Gharama kubwa ya kutokufaulu mipango yako ni kupoteza utulivu wa MUNGU kukusemesha

✅Wengi wakisha kopa kwenye kulipa ulipa nusu na nusu wanaweka mfukoni wanasahau MUNGU ndiye aliwafundisha kupata faida na au walipewa kibali cha kupata mkopo

✅Usije ukasahau na kusema huu utajiri ni nguvu zangu wakati ni MUNGU ndiye aliyekupa nguvu za kupata utajiri

UNAFIKIRI KWANINI MUNGU ALILETA SADAKA
▶Si kwamba ana shida na pesa yako
▶Lengo la kwanza lilikuwa kutumia sadaka kukutengenezea FIKRA sahihi ndani yako
✳Tazama maana ya
⚫Malimbuko=MUNGU anataka umfikirie yeye kwanza
⚫Zaka ya kwanza=MUNGU anataka kupewa heshima ktk maisha yako

✅Watu wengi kwenye kipindi kigumu na chenye kibano wako tayari kutafuta hela kulipa Benki lakini si kwa MUNGU. Kwa MUNGU excuses zitakuwa nyingi sana na hata kusema "MUNGU we si unajua nilivyobanwa"

✅MUNGU hana maana wala hataki kukufirisi bali anataka kukutengenezea FIKRA zenye Nidhamu

✅Jifunze kumpa MUNGU 100% naye anakurudishia 100%

✅Muulize MUNGU kwanza kwenye kila kitu, ratiba zako, muda wako na mambo yako mkabidhi na mfikirie MUNGU kwanza

✅Usitamani kuiga maisha na FIKRA za mtu mwingine hakikisha MUNGU anakupa mbinu za kujenga FIKRA za kwako mwenyewe.

✅FIKRA zenye kujenga nidhamu ndani yako.zitakufanya utende haki wala hazitakupeleka kwenye kupokea rushwa

✅FIKRA hizi zitakuwekea unyenyekevu ndani yako, kujishusha na kujifunza kutoka kwa wengine

✅Usijaribu ku copy na ku paste kutoka kwa mtu mwingine BWANA atakupa mikakati sahihi ndani yako

MAOMBI


**SIKU YA TANO**

No comments:

Post a Comment