.

.

.

.

Wednesday

NA IKAWE NURU: NA NIKAJUE NINI HASA NIPASWACHO KUFANYA.

 “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.” (MWA. 1:1-3 SUV). 

Hapo mwanzo kabisa Mungu alipoziumba mbingu na nchi kila alichokiumba kilikuwa kamili pasipo kasoro. 

Kuna kitu kilitokea ambacho bibilia imeamua kunyamaza kimya ambacho kilisababisha hizo mbingu na nchi zilizoumbwa katika hali ya ukamilifu pasipo kasoro ziwe ukiwa na utupu, na hiyo hali ya ukiwa na utupu ilifanywa mbaya zaidi na hali ya giza lililofunika uso wa vilindi vya maji. 

Pamoja na uwepo wa Mungu juu ya uso wa maji, hamna ambacho kingeweza kufanyika alimradi giza lilikuwepo juu ya uso wa vilindi vya maji. Mungu alipotaka kushughulika na hali ya utupu na ukiwa kitu cha kwanza ambacho ilibidi ashughulike nacho ni hilo giza ambalo lilikuwa linaipa nguvu huo ukiwa na utupu. Mungu akasema iwe nuru

Kutoka Kwa Pastor Carlos Kirimbai.

No comments:

Post a Comment