.

.

.

.

Thursday

Mchungaji apoteza watoto wanne katika ajali yeye na mkewe wasalimika


Kama kuna jambo limefichwa usoni pa wanadamu ni KIFO Tungelijua sijui tungekuwa na aina gani ya Maisha.Labda tusingesoma,labda tusingejenga nyumba,labda tusingeoa na kuolewa,labda tusingezaa watoto na yamkini tusingenunua magari wala kusafiri kwa kutumia magari hayo...inabaki kuwa fumbo!

Jana ilikuwa siku ngumu na mbaya ambayo itabaki kuwa kovu kwa maisha yote kwa Rev.Dr Pastory Michael Majembe ambaye ni mchungaji wa TAG-Ebenezer(Dodoma)Mwanataaluma mahiri wa Theolojia,na Mwalimu wa Chuo biblia Dodoma(Central Bible College,zamani AGBC)na familia yake,Kanisa la TAG kwa ujumla,ndugu jamaa na marafiki...baada ya kupata Ajali ya Gari akiwa na familia yake,siku ya jana katikati ya Mtera na Mpunguzi,Mkoani Dodoma na Kupoteza Watoto wake Wanne kwa pamoja Junior,Isack,Gabriel na Glady katika ajali hiyo.Mchungaji Pastory Majembe na Mama Bwana amewaponya,bado wanahitaji maombi maana nao wamepatwa na Majeraha na wanaendelea na matibabu.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe

Picha ya Mchungaji,Mke wake na marehemu watoto wake waliofariki katika ajali hiyo
No comments:

Post a Comment