.

.

.

.

Monday

Askofu Shayo: Ombeeni mazunguzo ya muafaka Z'bar

Askofu wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Augustino Shayo, amewataka wakristo kuendelea kuomba ili mazungumzo ya viongozi wakuu wa visiwa hivyo kuhusiana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu yakamilike kwa  amani na kupatikana muafaka.

Amesema nibudi kila mwananchi kusikiliza hatma ya mazungumzo hayo na kuwataka kuaacha  kushabikia masuala yasio ya msingi ambayo yanweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Akizungumza wakati akitoa mahubiri ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha  mwaka 2016  katika Kanisa la Mtakatifu  Francis, Chakechake, Pemba, mwishoni mwa wiki, Askofu Shayo pia aliwashukuru  waumini wa kanisa hilo kwa maombi yao yaliyo fanikisha uchaguzi mkuu Tanzania kuwa wa amani na kuwataka kuendelea kuomba ili hatma ya uchaguzi wa Zanzibar  ipatikane kwa njia ya amani na upendo.

“Keshini mkiomba ili mazungumzo ya viongozi wa siasa yakamilike na yawe ya amani na utulivu kwa maslahi ya wananchi wa Zanzibar,” alisema.

Aidha, Askofu Shayo aliwasisitiza waumini wa dini hio kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu mwaka huu.

Alisema mwaka 2015 kiwango cha elimu Jimbo Katoliki Zanzibar kilishuka, hivyo juhudi za makusudi  zinahitajika kuchukuliwa ilikuboresha sekta hiyo.

Amesema mwaka wa 2014 idadi ya shule za maandalizi zilizokuwa zikisimamiwa na kanisa hilo Zanzibar ilikuwa 28, lakini zimepunguwa hadi 18 mwaka 2015.

“Idadi ya skuli za maandalizi zimeshuka hadi kubaki 18, nyingine zimepungua kutokana na makosa ya wanafunzi jambo ambalo linahitaji kubadilika mwaka huu wa 2016,” alisema

CHANZO: NIPASHE 

No comments:

Post a Comment