.

.

.

.

Thursday

NAMNA YA KUPATA ALAMA YA UBORA (TBS)

Ili mfanyabiashara ama mzalishaji aweze kuuza bidhaa, ama huduma yake kwa 
usalama na bila usumbufu anahitaji kuwa na alama ya ubora katika bidhaa yake (tbs). 
Kwani alama hii ndio ikatayo thibitisha usalama na ubora wa bidhaa hiyo. Alama hii 
hutolewa na shirika la viwango Tanzania kama moja ya skimu ya kudhibiti ubora wa 

Pastor,Adv Justine Kaleb

Ili mzalishaji aweze kuwa na alama ya ubora katika bidhaa yake anatakiwa kumiliki 

leseni ya alama ya ubora kutoka shirika la viwango Tanzania (TBS). hivyo basi, zipo 

hatua mbalimbali ambazo mzalishaji hupaswa kuzingatia kabla ya kupata leseni ya 

kutumia alama ya ubora ya TBS kwenye bidhaa yake.

Hatua ya kwanza ni maombi ya uthibitishaji ubora ambayo hufanywa na mwombaji 

kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la viwango Tanzania kwa maandishi. Majibu 

hutolewa yakielezea taratibu za kufuata na gharama zote zinazohitajika. 

Majibu hayo huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji huijaza na kuirudisha 

TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo: mtiririko wa uzalishaji wa bidhaa husika, mfumo 

wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora, orodha ya malighafi anazotumia na 

mahali zinakotoka kwa kila bidhaa pamoja na ramani inayoelekeza jinsi ya kufika 

kiwandani kwake. 

Baada ya kutekeleza na kuwasilisha nyaraka hizo, tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali 

hupangwa. Izingatiwe kuwa mwenye kiwanda anatakiwa kuwa katika uzalishaji siku ya 

kufanya ukaguzi wa awali.

Hatua inayofuata ni ukaguzi wa awali, ambayo ufanywa na wakaguzi wa TBS. ambapo 

sampuli uchukuliwa na kupimwa ili kuona kama bidhaa inakidhi matakwa ya kiwango 

husika. Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili 

kurekebishwa.

Hatua ya tatu ni upimaji wa sampuli zilizochukuliwa, na upimaji huo unafanyika katika 

maabara za shirika la viwango Tanzania kwa kufuata kiwango husika. Baada ya kazi ya 

upimaji kumalizika, ripoti hutolewa kwa mwombaji.

Hatua ya nne na ya mwisho ni utoaji wa leseni: uamuzi kuhusiana na kutoa ama 

kutotoa leseni ya kutumia alama ya ubora hutegemea tu ripoti ya ukaguzi wa awali wa 

kiwanda pamoja na ripoti ya maabara. 

Kimsingi ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba mazingira ya uzalishaji 

kiwandani, mfumo wa uzalishaji na bidhaa iliyopimwa havina matatizo. Ikiwa sivyo basi 

mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena 

na kuleta sampuli nyingine.

Vilevile, serikali imejaribu kutenga fungu kila mwaka kwa ajili ya wajasiriamali wadogo 

na wa kati na kati ya hao wajasiriamali hao wanaweza samehewa kulipa ada yoyote 

wanapoomba bidhaa zao kuthibitishwa ubora. 

Hivyo basi, mjasiliamari ili kuweza kupata msamaha huo anatakiwa kupata barua ya 

utambulisho kutoka ofisi ya SIDO iliyokaribu au chama cha wazalishaji mfano TAFOPA. 

Taarifa fupi kutoka idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA 

kwa wale wanajihusisha na uzalishaji wa chakula huhitajika. 

Muda wa alama ya leseni hiyo hudumu kwa mwaka mmoja. Na baada ya kupata leseni 

ya kutumia alama ya ubora wanapaswa kutunza taarifa za uzalishaji na mauzo ambazo 

zitahitajika kwa ajili ya ukaguzi wa baadae ukataofanywa na shirika.

Ili uendelee kudumu sokoni na kufanikiwa sana kibiashara alama hii ya ubora ni kitu 

muhimu sana  kwako mzalishaji na mteja pia.


KWA MAWASILIANO|;

ADVOCATE JUSTINE KALEB
CEO/LEGAL CONSULTANT
MORIAH LAW  CHAMBERS,
MAVUNO HOUSE - POSTA MPYA,
(OPPOSITE TO GAPCO PETROL STATION),
1ST FLOOR - OFFICE NO. 102,
P.O. BOX 70849,
DAR ES SALAAM - TANZANIA - EAST AFRICA.
MOB: +255 755 545 545 600 / +255 713 636 264
TEL: +255 222 110 684
FACEBOOK: Moriah Law Chambers

No comments:

Post a Comment