.

.

.

.

Monday

Pastor Emmanuel Myamba aaga Ukapera,afunga ndoa huko Zanzibar

 Msanii wa Bongo Movie Emmanuel Myamba alimaarufu Pastor Myamba ameamua kuanza maisha mapya ya ndoa baada ya kufunga ndoa na mchumba wake huko Zanzibar wikiendi iliyoisha.

Sio movie wala maigizo bali ukweli ni kwamba Mwigizaji huyo wa Bongo Movie Emmanuel Myamba anayezitendea haki scene za uchungaji, ameaga rasmi maisha ya ubachela baada ya kufunga pingu za maisha na mchumba wake wa kipindi kirefu aitwae Praxceda.

Akionekana kuwa mwenye furaha isiyo na kifani, Myamba aliweza kushea baadhi ya picha za ndoa yake kwenye ukurasa wake wa Facebook ikiwemo zawadi ya kitita cha pesa zilizokuwa zimewekwa kwenye kitololi walizozawadiwa na wanakamati.

Mr & Mrs Myamba
Zawadi ya pesa aliyopewa na wanakamati wenzake katika harusi hiyo


No comments:

Post a Comment