.

.

.

.

Monday

Kongamano la Viwango vya Juu Living Water Center lafanyika baraka

Zilikuwa ni siku sita za kwenda viwango vya juu katika Jiji la Dar es salam Katika Kanisa la Living Water center chini ya Mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi Katika Kongamano liloitwa Kongamano la Viwango vya Juu (Higher Levels Conference) 

Katika Kanisa la Living Water Center kila mwaka huwa kuna Kongamano kuu linakuwa na watumishi wa Mungu kutoka Makanisa mbalimbali Nchini na nje ya Nchi,kwa mwaka huu alikuwepo Bishop Kameta Dar es salaam,Bishop Oram Mustafa kutoka Arusha Tanzania, Mchungaji Titus Mkama wa Ilala TAG Dar e salaam, Bishop Dr Peter Muteba South Afrika,Bishop Dr.Tengu Yoka kutoka NairobiApostle Aaron Timoth DRC, Dar es salaam Tanzania na wenyeji Apostle Onesmo na Lilian Ndegi.


Watu walipata muda wa kutosha kujifunza Neno la Mungu kwa ufasaha na kuombewa na watumishi wote waliohudumu  katika Kongamano hilo

Living Waters Praise Team,Totoo,Kwaya kutoka Glory Land Arusha,na Kwanya kutoka Nairobi  ndio walihudumu  katika Kongamano hilo,King Chavala naye alikuwepo kufanya vitu vyake!

 Apostle Onesmo Ndegi mwenyeji wa Kongamano hilo

Bishop Oram Mustafa kutoka Arusha Gloryland International Church
Mchungaji Titus Mkama wa Ilala TAG Dar e salaam
Bishop Dr Peter Muteba South Afrika

Bishop Dr.Tengu Yoka kutoka Nairobi

Living Waters Praise Team walipokuwa wakihudumu katika Kongamano hilo
Katika Siku ya mwisho wa Kongamano hilo kulkuwa na tendo la kumfanya Bishop Dr Peter Muteba South Afrika kuwa mzee wa heshima pia kuingia katika Agano na mtumishi huyo no na uhusiano wao katika Kanisa la Living Water Center kama wanavyonekana katika picha
Bishop Dr Peter Muteba South Afrika akipokea zawadi ya picha iliyochorwa kwa mkono

Champagne kama ishara ya kujipongezaTotoo Mwanamziki Kutoka South AfrikaWatumishi waliohudumu katika Kongamano hilo,wakwanza  Kushoto ni Apostle Aaron Timoth kutoka DRC,anayefuatia mwenye suti ya kaki ni Bishop.Dr Tengu Yoka kutoka Nairobi Kenya,kisha Bishop.Dr Peter Muteba Afrika kusini, mwenye shati jeupe ni Apostle Onesmo Ndegi mwenyeji,mwisho kulia Bishop Oram Mustafa kutoka Arusha Tanzania.
Wakwanza ni mama Apostle Ndegi akiwa na baadhi ya wake wa watumishi walihudumu katika Kongamno hilo


No comments:

Post a Comment