.

.

.

.

Wednesday

Anglikana laridhia wanawake Maaskofu


Kanisa kuu la Anglikana Uingereza
Maafisa katika kanisa hilo wanaamini wana ufuasi mkubwa unaounga mkono hoja hiyo.Sasa baada ya kupitishwa kwa kura hiyo, huenda askofu wa kwanza mwanamke akachaguliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Makasisi wanawake walio thuluthi moja ya viongozi wa kidini wa kanisa la kianglikana, wanasema haki sawa itawapandisha hadhi katika makanisa.

Hatua hiyo inemaliza mvutano wa miaka mingi na kuvunja utamaduni wa makarne katika kanisa hilo. Tofauti nyingi zimeibuka kuhusu suala hilo na hata kusababisha migawanyiko katika kanisa hilo ambapo baadhi ya ma dayosisi yameshawatawaza maaskofu wanawake, na kukaidi amri la hapo awali la kanisa kuu.Nchi zilizo na maaskofu wanawake:New Zealand,Australia,Marekani,Canada na Afrika Kusini

Kasisi Moses Bushendich kutoka kanisa la Kianglikana Uganda ameambia BBC kuwa misimamo imegawanyika juu ya maaskofu wanawake kutokana na mafundisho ya Bibilia.

''Kanisa la Afrika halina uamuzi wa pamoja juu ya suala hili. Kila tawi limechukua msimamo wake baadhi wanapinga na wengine wanaunga mkono'' amesema kasisi Bushendich.

Baadhi ya itikadi ambazo zimekuwepo kwa miaka m ingi katika makanisa kuu kama vile Katoliki na Anglikana ni wanawake kuwa maaskofu wanawake, na kruhusu ndoa ya wapenzi wa Jinsia moja ambayo tayari baadhi ya maumini na maaskofu wa kanisa hilo wamepigia debe kuidhinishwa.

No comments:

Post a Comment